TUME
ya kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) kwa kushirikian na shirika la UNICEF pamoja na
kituo cha Clouds Radio mwishoni mwa wiki wamezindua kipindi maalumu cha redio kijulikanacho
kama “Shuga” mahsusi kwa vijana kikilenga kuwawezesha kuongea na kuwasiliana kuhusu jinsi ya
kujikinga na maambukizi ya VVU na UKIMWI.
Kamshna wa TACAIDS Bi Faraja Kotta Nyalandu akiashiria uzinduzi wa programu ya Shuga mahsusi kwa kuwalinda vijana na maambukizi ya VVU kupitia Redio Clouds juzi huko Kinondoni, Biafra |
Uzinduzi
huo ulifanyika katika viwanja vya Biafra, Kinondoni, nje kidogo ya jiji la Dar
es salaam.
Shuga
kinalenga kuchochea maongezi miongoni mwa vijana kuhusu VVU na UKIMWI kwa kutoa
burudani na elimu ambayo itakuwa inawaasa kuhusu hatari zinazowakabili kama
hawatachukua tahadhari inayofaa
Ni
mtiririko wa vipindi 12 ambavyo vitarushwa na redio Claud FM ya Dar es salaam
pamoja na ile ya Kitulo FM ya Makete, mkoani Njombe. Lengo ni kufikia ndoto ya
kitaifa ya kufuta kabisa kabisa maambukizo
ya VVU miongoni mwa watanzania hadi
kufikia sifuri ifikapo mwaka 2015
Mwakilishi Mkazi wa UNICEF nchini Dk.Jama Gulaid akisoma hutoba wakati wa uzinduzi huo |
Mgeni
wa Heshima katika hafla hiyo—Mwenyekiti Mtendaji wa TACAIDS Dk Fatma Mrisho—ambaye
aliwakilishwa na Mkurugenzi wa Ulaghibishi na Habari wa Tume Bw. Jumanne Issango
alisema uzinduzi wa Shuga ulikuwa muhimu na umekuja wakati muafaka katika kipindi
ambacho maambukizi ya VVU miongoni mwa vijana yalikuwa yanaongezeka.
Kasema,
kila siku kuna mambukizi mapya 2,500 miongoni mwa vijana duniani kote, wanne kati
ya kumi wanatoka Kusini mwa Jangwa la Sahara (SSA) ambapo ndipo wengi wa vijana
hawa wa kike na kiume wanatoka
Baadhi ya wakazi wa Biafra wakifuatilia uzinduzi huo |
Mwelekeo
kama huo umejionesha Tanzania kwa mujibu wa ushahidi wa hivi karibuni, akasema
Dk Jama Gulaid—mwakilishi mkazi wa UNICEF nchini wakati wa hafla hilo iliyohudhuriwa
na mamia ya wakazi waeneo hilo lililo
karibu na Chuo Kikuu Huria (OUT).
Programu
ya Shuga ni mfano wenye matumaini wa ushirikiano kati ya taasisi za umma, na binafsi kwa kufanya kazi pamoja na vijana
ili kuchangia katika jitihada za kupunguza maambukizo mapya ya VU, alisema Dk
Jama na kuongeza: Shuga ni kipindi ambacho kitajikita katika kuchochea
mabadiliko ya tabia. Ni kipindi kitakachobainisha vichocheo vya mambukizi ya
VVU miongoni mwa vijana na kutoa mwangaza wa namna ya kupata huduma za ushauri
nasaha, upimaji na matumizi ya kondomu.
Baadhi ya washiriki wa uzinduzi huo |
Kwa
mujibu wa matokeo mapya kabisa ya Utafiti wa Kitaifa kuhusu mwelekeo wa UKIMWI
na Malaria (THMIS, 2012) kumekuwa na kupungua kidogo kwa maambukizi miongoni mwa watanzania wenye umri kati ya miaka 15
na 49. Hii ni kutoka asilimia 7 mwaka
2003 hadi asilimia 5.1 mwaka 2012
Hata
hivyo, kwa mujibu wa Dk Mrisho, kiwango cha mambukizi bado kiko juu ikiwa ni
takribani ya wastani wa watanzania 80,000 wanaoambukizwa kila mwaka.
“Hakika
naamini kwamba ubunifu huu ambao unawaunganisha vijana na wadau wengine katika
vita hii ndio unaotakiwa hapa kwetu ili kutuwezesha kufikia lengo la maambukizo
sifuri,” alisema Dk Mrisho.
Umma ukifuatilia matukio uwanjani hapo |
Mkurugenzi
wa Clouds Radio Bw. Joseph Kusaga,alisema ushirikiano
huo ulikuwa wa kutia moyo na kuahidi kutumia tasisi yake kuendelea kutoa elimu
sahihi na elimishi kwa lengo la kuwasaidia vijana kuwa na afya bora hadi
kufikiaa utu uzima
Wageni waalikwa |
Naye Bi Faraja
Kotta Nyalandu ambaye ni Kamishna wa Tume pamoja na kuwa balozi wa Shuga akawaataka vijana wasikubali
kuuza mechi. Kwa mujibu wa Bi Nyalandu kauli mbiu ya “kijana usiuze mechi”
alilenga kuwaasa vijana kuchukua tahadhari wakati wa mahusiano ya kingono.
Bi Vicky Chuwa akimwongoza Mwakilishi wa UNICEF kutoka jukwaani |
Uzinduzi huu
unaashiria utekelezwaji wa mkakati wa mataifa kadhaa ya kikanda uliosimamiwa na
ya UNICEF, Multi-Media Television (MTV) na Kizazi kisichokuwa na UKIMWI wa PEPFAR
sasa unaridhiwa katika maudhui ya kitanzania.
Kiduku |
0 comments:
Post a Comment