Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NACP), mwishoni mwa wiki, ulizindua mwongozo wa Taifa wa Kupitia na Kuhakiki Nyenzo za habari, elimu na mawasiliano ya kubadili tabia kwa lengo la kuboresha habari na mawasiliano yanayofanywa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na wadau wake kwa lengo la kuthibiti kuenea kwa virusi vya UKIMWI (VVU).
NACP iliyopo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ikiwa na jukumu la kusimamia masuala ya kinga, tiba, matunzo na misaada kwenye nyanja ya UKIMWI katika sekta ya afya ncini, imezindua mwongozo huo kwa wadau wa habari, elimu na mawasiliano (IEC) na mawasiliano ya Kubadili Tabia (BCC), mjini Bagamoyo.
Mwongozo huo wa kwanza kwenye sekta ya afya unalenga kuweka viwango vya kitaifa ambavyo wadau wa mawasiliano ambapo nyenzo zote za machapisho na za kielektroniki za IEC/BCC zitapaswa kuhakikiwa na idara hiyo kwa lengo la kuboresha ujumbe inayotolewa.
Lengo kubwa la mwongozo huo ni kuhakikisha matangazo yote yanayohusu kinga, tiba, matunzo na misaada kwenye nyanja ya UKIMWI yanahakikiwa ubora ili kutoa ujumbe sahihi kwa walengwa katika jitihada za serikali za kuunga mkono jitihada za wadau wanaojihusisha na afua za ugonjwa huo nchini.
Katika dibaji ya mwongozo huo, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Donan Mmbando anasema licha ya juhudi kubwa ya uenezaji na upataji wa shughuli za habari na mawasiliano kuhusu VVU na UKIMWI nchini, bado kuna baadhi ya ujumbe usio sahihi unaotolewa kwa walengwa.
"Ujumbe huo unatofautiana bado ni tatizo kubwa kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika jitihada zake za kutokomeza maambukizo mapya ya VVU pamoja na kutoa matunzo, matibabu na msaada kwa watu wanaoishi na VVU," anasema katika dibaji hiyo na kuongeza;
"Hali kadhalika usanifu wa viwango visivyofaa vya nyenzo zinazotayarishwa, wakati mwingine hufanya iwe vigumu kwa ujumbe kufikishwa kwa usahihi kwa walengwa waliokusudiwa.
Awali, akimkaribisha mgeni Rasmi katika mkutano huo, kaimu mkuu wa kitengo cha habari elimu na mawasiliano cha NACP, Ndg. Baraka Mpora alisema mwongozo huo umetokana na miongozo ya kitaifa ya kuongeza ubora wa huduma za VVU na UKIMWI iliyotayarishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuhakikisha uongezaji ubora wa afua zote kuhusiana na ugonjwa huo unatekelezwa kwa uwiano bora.
Nyenzo zote za machapisho na za elektroniki za IEC/BCC zimekuwa na mikakati mikuu ya inayotumika kuwapasha habari na kuwaelimisha walengwa ili kuinua kiwango cha cha uelewa kuhusu VVU na UKIMWI na kuhimiza makubaliano ya tabia utakaosaidia kupunguza maambukizo mapya ya VVU na maambukizo ya magonjwa ya ngono (STI).
Wakati wa kuongoza mapitio ya mwongozo huo Afisa Habari na Mawasiliano wa NACP, Shoko Subira amesema mwongozo huo pia unatoa maelekezo ya usahihi wa matumizi ya nembo inayotumika ikiwa ni pamoja na uwekaji wa nembo ya serikali.
"Kumekuwa na tatizo la jinsi ya kuweka nembo lakini kwa mwongozo huu umeagiza Nembo ya Serikali iwekwe juu ya nembo nyingine au iwe ya kwanza kushoto iwapo nembo zitawekwa kwa ulalo na kufuatiwa na nembo zingine kwa kuwa nembo hii ni alama ya kitaifa na ni kubwa kwa hadhi kuliko nyingine," akasema Shoko
Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa NACP Bw. Baraka Mpora akitoa utambulisho wa mwongozo huo kwa wajumbe |
Sehemu ya wataalam wa mawasiliano na habari wakisikiliza kwa makini mtoa mada (hayupo pichani) |
Lengo kubwa la mwongozo huo ni kuhakikisha matangazo yote yanayohusu kinga, tiba, matunzo na misaada kwenye nyanja ya UKIMWI yanahakikiwa ubora ili kutoa ujumbe sahihi kwa walengwa katika jitihada za serikali za kuunga mkono jitihada za wadau wanaojihusisha na afua za ugonjwa huo nchini.
Dk Mapunda akitoa nasaha wakati wa ufunguzi wa mkutano huo |
"Ujumbe huo unatofautiana bado ni tatizo kubwa kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika jitihada zake za kutokomeza maambukizo mapya ya VVU pamoja na kutoa matunzo, matibabu na msaada kwa watu wanaoishi na VVU," anasema katika dibaji hiyo na kuongeza;
Majadiliano katika vikundi |
Awali, akimkaribisha mgeni Rasmi katika mkutano huo, kaimu mkuu wa kitengo cha habari elimu na mawasiliano cha NACP, Ndg. Baraka Mpora alisema mwongozo huo umetokana na miongozo ya kitaifa ya kuongeza ubora wa huduma za VVU na UKIMWI iliyotayarishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuhakikisha uongezaji ubora wa afua zote kuhusiana na ugonjwa huo unatekelezwa kwa uwiano bora.
Nyenzo zote za machapisho na za elektroniki za IEC/BCC zimekuwa na mikakati mikuu ya inayotumika kuwapasha habari na kuwaelimisha walengwa ili kuinua kiwango cha cha uelewa kuhusu VVU na UKIMWI na kuhimiza makubaliano ya tabia utakaosaidia kupunguza maambukizo mapya ya VVU na maambukizo ya magonjwa ya ngono (STI).
Dk Jesse kutoka Muhimbili akitoa mada kwa washiriki |
"Kumekuwa na tatizo la jinsi ya kuweka nembo lakini kwa mwongozo huu umeagiza Nembo ya Serikali iwekwe juu ya nembo nyingine au iwe ya kwanza kushoto iwapo nembo zitawekwa kwa ulalo na kufuatiwa na nembo zingine kwa kuwa nembo hii ni alama ya kitaifa na ni kubwa kwa hadhi kuliko nyingine," akasema Shoko
0 comments:
Post a Comment