Sunday, February 23, 2014

Wanafamilia nchini wafundwa kuhusu UKIMWI

Kamishna wa TACAIDS Sheikh Hassan Kiburwa akipima VVU katika banda la upimaji lililosimamiwa na AMREF wakati wa siku ya  familia ya wafanyakasi wa Tume jana
IMEELEZWA kwamba asilimia nane ya wanandoa wanaoishi na virusi vya UKIMWI (VVU) ni ile mwenzi mmoja kuwa na maambukizi wakati mwingine hana maarufu kama “discordant couple”
Akizungumza katika hafla ya Siku ya Familia ya watumishi wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Mwenyekiti Mtendaji wa tume hiyo, Dk. Fatuma Mrisho ametoa wito kwa wananchi kupima afya zao.
Mwelimishaji kuhusu masuala ya familia Bw. Chalila akitoa somo katika siku ya familia ya wana Tume
“Kitendo cha walio katika ndoa kutegeana kupima, mfano, mmoja kuona yuko salama na mwingine kuamini na yeye yuko salama, kinarudisha harakati za kitaifa za kukomesha maambukizo mapya ya VVU,” amesema Dk Mrisho
Amesema watu wengi hawajapima, hali inayofanya jitihada za kukabiliana na maambukizo ya VVU kuwa ngumu na kuisisitiza ujumbe wake kwa walio katika ndoa kuwa wako kwenye hatari sawa na wasio kwenye ndoa ya kupata maambukizo.
Wanafamilia
Dk. Mrisho ameyataja makundi mengine yenye kiwango cha juu cha maambukizo kuwa ni wanaotumia dawa za kulevya kwa kujidunga sindano kwani utafiti zinaonyesha nusu yao wanaishi na VVU.
Kikundi cha ngoma kikiburudisha
Akizungumzia utafiti mdogo uliofanywa katika Kata ya Kimara jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Dk Mrisho amesema utafiti huo uligundua kati ya sindano 10 zilizotumiwa na watumia dawa za kulevya, saba zilikutwa zina virusi hivyo vinavyosababisha UKIMWI.
Ameyataja makundi mengine ambayo tafiti zimegundua kuwa na viwango vya juu vya maambukizo kuwab ni watu wenye wapenzi wengi pamoja na wanaofanya au kushiriki katika kuuza ngono.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya PM Bi.Regina Kikuli akikata keki ya Tume kama ishara ya kuunga mkono malengo ya sifuri tatu dhidi ya VVU na UKIMWI
Mapema, akitoa mafunzo kwa wanafamilia wa TACAIDS, mwezeshaji, Simon Chanila alisema kukosekana kwa uaminifu katika ndoa ni sehemu ya changamoto.
Chanila amesema kukosekana uaminifu katika ndoa kunasababishwa na kukosekana kwa uwazi, uaminifu, tamaa, kutotimiziwa matarajio ya mmoja, kukosekana kwa mawasiliano pamoja na ndoa za kulazimishwa.
Wanafamilia wa TACAIDS wakiselebuka
Aliwaambia wana familia hao kwamba ili ndoa zidumu, wanapaswa kuzingatia kanuni 14 alizowaambia zikiwa ni pamoja na kumshirikisha Mungu katika hatua zote za mahusiano yao.
Kanuni nyingine ni wenza kujitengea muda, kuonyesha kujaliana, kujali tendo la ndoa, kuwa wazi, kumpenda na kumsifia mwenzake wa ndoa pamoja na kutotilia maanani watu nje ya muunganiko wao.
Msanii "Nyerere" akibadilishana na mwana-TACIDS Elisha Mngale
Chanila ametaja kanuni nyingine ni kujua majukumu, kushirikiana pamoja na kuomba msamaha na kusamehana.
Katika tuko hilo, vijana na watoto wa familia ya TACAIDS nao pia walipewa mafunzo kwa niaba ya wana rika wenzao nchini.
Mama na mwana
Mmoja wa wakufunzi kutoka tume hiyo Bw. Hatibu Kunga aliwataka vijana hao kuzingatia maadili mema ya maisha kama njia kuu ya kuepuka kuambukizwa VVU
Akipokezana na Mkurugenzi wa mwitikio wa taifa kuhusu UKIMWI wa Tume Bw. Morisi Lekule, mwezeshaji huyo alisema badala ya kujiingiza katika vitendo hatarishi wakati wa ujana, badala yake wajikite katika shughuli za mazoezi baada ya kazi za darasani na nyumbani ili miili yao iwe na afya na kutokuwa na vishawishi vyovyote vibaya.
Mwelimishaji kuhusu kinga ya VVU Bi Noela Mbeyela kutoka T-MARC akiwa na wageni waliotembelea banda lake jana katika siku ya familia ya TACAIDS.
Mbali na mafunzo hayo, pia kulikuwa na shughuli sa upimajin wa afya, VVU na msukumo wa damu (presha) ambazo ziliendeshwa na wataalamu kutoka AMREF, T-MARC na taasisi nyingine zilioalikwa.
Moris Lekule akimwaga somo kwa vijana wana-familia ya TACAIDS. "Fanyeni excersise" muepukane na tamaa

0 comments:

Post a Comment