Thursday, September 26, 2013

Vita Dhidi ya UKIMWI nchini: TACAIDS yatoa hali halisi

Mwenyekiti Mtendaji wa TACAIDS Dk.Fatma Mrisho (katikati) akisikiliza swali kutoka kwa mwandishi (hayupo pichani) wakati viongozi wa tume walipokutana na wahariri juzi ili kutoa hali halisi ya UKIMWI nchini
NCHI  wanachama wa Umoja wa Mataifa (UwM) (Tanzania ikiwemo) zilikutana jijini New York, Marekani tarehe 10 June 2011 na kukubaliana malengo makuu ya UKIMWI ambayo kila moja ya nchi zilizohudhuria zitajitahidi kuyafanya. Mkutano ulihudhuriwa na wakuu wa nchi 30 na kuhudhuriwa na washiriki 3,000. Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Mhe Gharib Bilal, Makamu wa Rais. Mapema wiki hii, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya UKIMWI Nchini (TACAIDS) Dk. Fatma Mrisho aliliongoza jopo la timu yake kukutana na wahariri wa habari nchini ili kuwapa hali halisi ya kampeni dhidi ya ugonjwa huo kama ilivyoagizwa katika mkutano wa Marekani, takribani miaka mitatu iliyopita.

Kupunguza  maambukizo ya UKIMWI yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana.

Maambukizi yanapungua, ikiwemo maambukizi mapya, kupungua huku sio kukubwa kama ilivyotakiwa kuwa (7% 2003/04, 5.7% 201/08 na 5.3% 2011/12); miaka yote wanawake wana maambukizi zaidi ya wanaume, mijini maambukizi ni zaidi ya nje ya mji. Kwa miaka ya karibuni maambukizi kwa wanawake yameshuka kwa kiwango kidogo sana.

Kupunguza  maambukizi kwa watu wanaojidunga sindano za dawa za kulevya.
Wahariri wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti Mtendaji wa TACAIDS juzi
Taarifa zilizopo ni chache, lakini hizi chache zinaonesha kuwa wanajidunga sindano za madawa ya kulevya wana maambukizo ya UKIMWI kwa kiwango cha 12.3% hadi 42% hiki ni kiwango kikubwa zaidi kuliko wastani wa Taifa ambao ni 5.3%. lengo ni kupunguza maambukizi haya kwa nusu ya kiwango cha 2010. Wanaume wanaojamiana na wanaume wenzao wana maambukizo ya UKIMWI  kiwango cha 51/%, na wanawake wanaouza ngono Dar es salaam maambukizo ya UKIMWI ni 42%, wanawake wanaotumia njia ya nyuma kujamiiana wana hatari hiyo  hiyo. 

Kutokomeza maambukizi ya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto 

Lengo ni kufikia kiwango cha chini ya 5% ya maambukizo ya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa  mtoto (kutoka kwenye kiwango cha 18%). Wanawake wengi (85%) wajawazito wanapimwa na wanaopatikana na maambukizo hupatiwa dawa za kinga kwa watoto pamoja na wao kutumia dawa kupunguza makali ya maambukizo ya UKIMWI. Kuna mafanikio yanaonekana kutoka wastani wa watoto 26,000 walioambukizwa 2009 kufikia 15,000 mwaka 2012. Huduma nyingi za Mama na mtoto (93%) zinaunganisha pia huduma hii ya kuzuia maambukizo kutoka kwa mama kenda kwa mtoto.
Sehemu ya wahariri wakisikiliza mawasilisho kutoka kwa viongozi wa tume
Kufikia lengo la kuwa na watu 1.5 million walianza na kuendelea kutumia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (ARV)

Kuna wastani wa watu 710,000 wanaishi na virusi vya UKIMWI ambao wamefikia kiwango cha kustahili kuanza kutumia ARVs. Idadi ya watu wanaofikiwa na kuanza kutumia ARV imekuwa inaongezeka kwa kasi, hasa kuanzia 2010; lengo ni kufikia  watu 700,000 ifikapo 2015, hadi 2012, tayari zaidi ya watu 663,911wamefikiwa. Wanawake ni wengi kuliko wanaume na pia imeokekana kwamab wanaume huchelea kuanza kutumia huduma za afya za UKIMWI. Ikiwemo kupima na piaa kuanza tiba. Serikali inazidi kuboresha ufikiwaji wa watoto ambao kwa sasa ni 25%, lengo ni kufikia 70% ifikapo 2017. 

Kupunguza vifo vitokanavyo na kufua kikuu (TB) kwenye watu waishio na virusi vya UKIMWI .

Lengo ni kupunguza nusu ya vifo kutikana na TB kwenye watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI ifikapo 2015. Huduma za TB na UKIMWI zimeunganishwa kwenye zaidi 90% ya huduma za afya. Kwenye watu ambao UKIMWI umechanganyika na TB, nusu  yao huenda wakapoteza maishsa kama  hawatiiwi ipasavyo. Inakadiriwa kwamba karibu ya 26% ya watu wanaomaambukizi yote mawili kwa wakati mmoja wanapatiwa tiba stahili. 
Wahariri
Kupunguza mahitaji ya rasilimali fedha za UKIMWI.

Mahitaji ya fedha ni mengi, kwa mwaka 2011/12 kumekuwa na kupungua rasilimali fedha ka kiwango cha 9%. Kutoka 2006/07 hadi sasa mgao ka sekta ya UKIMWI kwa nchi nzima umepungua kutoka ka zaidi. Wahisani wanaendelea kuonesha nia ya kutoa msaada kwa sekta hii, Serikali ya Marekani ikiongoza na kufuatiwa na Mfuko Maaluumu a UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu, Umoja wa Mataifa, Serikali z Canada, Denmark. Wastani wa 30% ya Halmashauri zimeanza kutenga fedha za UKIMWI kutokana na makusanyo ya Halmashauri, Tume ya kudhibiti UKIMWI inapendekeza kuwa lika Halmashauri ifanye hivyo ili ziweze kuhudumia yatima, wagonjwa w majumbani, kutoa huduma za kinga, kuboresha lishe kwa wahusika na kuwezesha wajane na yatima kuanzisha miradi ya kuongeza kipato na kupunguza utegemezi.
 
Kuondoa tofauti za kijinsia, uonevu na ukatili wa kijinsia, na kuongeza uwezo wa wanawake na watoto kujilinda na maambukizi wa UKIMWI.

38% ya wanaume wanaona ni sawa kwamba mume ana haki ya kumpiga mkewe kwenye mazingira Fulani. 61% ya wanawake  nchini waliachika /kutengana na mume/mwanamme wamewahi kupigwa, wanawake walioko kwenye ndoa 41% na hata ambao haawaajawahi kuwa kwenye ndoa 23% wameishapuigwa. Ngono ya kulazimishwa ni 20% yawnawake wa Tanzania wa umri wa miaka 15-49. Wengi wa wanawake hawa huwa wana hofu ya kwenda kwenye vyombo vya sheria, ijapokuwa sasa polisi wameanzisha dawati maalum la kutoa msaada stahili. Kuna haja ya elimu zaidi. Kwenye umri wa miaka ya 20-24, maabukizi kwa wanawake ni 4.4% ukilinganisha na wanaume ambao ni 1.7%
Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa Tume akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya fedha
Kuondoa kabisa unyanyapaa na ubaguzi unaolenga watu waishio na virusi vya UKIMWI

Unyanyapaa na ubaguzi bado ni kikwazo kikubwa nchini. Inaathiri ukubali wa kupima, ukubali wa kumwambia mwanafamilia, rafiki au kazini. Inaathiri pia utayari wa kuanza na kuendelea na dawa (ARVs), ukubali wa kutunza yatima, kujitangaza hadharani na kujiunga kwenye harakati za utetezi wa haki za watu wanaoishi na VVU. Unyanyapaa na ubaguzi pia unasababisha kuvunja haki za msingi za watu waishio na VVU (mfano mirathi, ulezi wa yatima, kuajiriwa na kuendelea kufanya kazi, upangaji wa nyumba, n.k).

Kuboresha mifumo ya kutolea huduma za UKIMWI kwenye sekta ya afya

Kwa kiwango kikubwa hili limewezekana, 93% ya huduma za mama na mtoto pia zinapima UKIMWI. Vituo vya upimaji vimeongezeka maradufu kwenye miaka ya karibuni. Dawa za ARVs zenye ubora zinapatikana. Kuna upungufu wa raslimali watu ambao serikali inautambua na kuna jitihada kubwa za kujaza mapengo.

0 comments:

Post a Comment