Saturday, September 28, 2013

Hivi kwanini wanaume tunazidiwa kupima VVU na wanawake?


Viongozi wa TACAIDS walipokutana na wahariri ofisini kwao
Kwa mujibu wa TACAIDS, kupima UKIMWI ni mlango wa kwanza wa kufanya maamuzi sahihi ya kujikinga na maambukizo ya Virusi Vya UKIMWI (VVU) na kuanza kutumia dawa za kupunguza maambukizo kama mpimaji atagundulika keshaambukizwa.
Takwimu zifuatazo zinaonyesha wanawake na wanaume waliopima na kujua hali zao za Afya kwa kila mkoa. Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa Taifa kuhusu UKIMWI na Malaria (THMIS) wa mwaka 2011/12

MKOA    WANAWAKE    WANAUME      
Arusha                64                     29      
Dar es Salaam    72                     55      
Dodoma              63                     42      
Geita                   50                     35      
Iringa                   69                     53      
Kagera                66                     44      
Katavi                  47                     42      
Kigoma                62                     53      
Kilimanjaro           64                     52      
Lindi                     74                     53      
Mara                     59                     50      
Morogoro              56                     36      
Manyara                56                     41      
Mbeya                   54                     42      
Mtwara                  71                     50      
Njombe                  74                     65      
Pemba                   55                     36      
Pwani                     72                     48      
Dk Raphael Kalinga, Mkurugenzi wa Sera na Mipango, TACAIDS
Ruvuma                  69                     51      
Shinyanga               61                    49      
Singida                    61                     51      
Tabora                     70                     52      
Tanga                      57                     48      
Unguja                     61                     52            
Takwimu hizo zinabainisha jinsi wanaume wasivyokuwa wajasiri kupima VVU katika kila mkoa. Hii maana yake nini?
Wataalamu wa masuala ya UKIMWI wanasema, mbali na unyanyapaa unaouzunguka ugonjwa huu, lakini pia wanaume wengi husubiria majibu ya wake zao wanapokuwa kliniki ya ujauzito. “Majibu ya mkewe yakitoka negative basi nae (mme) hujitapa na kujifariji kuwa naye yuko negative” aliwahi kuniambia mwanaharakati mmoja.
Mkuu wa kitengo cha Sera na Mipango katika Tume ya UKIMWI Nchini Dk Raphael Kalinga yeye huwa ana sera yake: UKIMWI Unaanza na Mimi. UKIMWI ni Janga langu Binafsi!
Kwa mujibu wa Dk Kalinga, hadi pale kila mtu bila kujali ameoa au ameolewa atakapotambua kuwa UKIMWI ni janga lake binafsi na kuchukua hatua za kujilinda yeye binafsi changamoto za kuukabili ugonjwa huo zitaendelea kuwepo.
"Hebu tufike mahali kila mmoja wetu atambue ugonjwa huu ni janga lake binafsi," akasema Dk Kalinga na kuongeza, tumwachie Rais ndie asema UKIMWI ni janga la kitaifa...Mkuu wa Mkoa aseme UKIMWI ni janga la Mkoa wake...Mkuu wa Wilaya naye aseme UKIMWI ni janga la wilaya yake...hivo hivo hadi ngazi ya famailia na hatimae mtu binafsi"
Dk Kalinga anasema, katika kufanikiwa katika juhudi za kutatua tatizo la UKIMWI nchini, kimakati inabidi ijengwe kutoka kwa mtu binafsi kwani suala la msingi katika mapambano ya UKIMWI ni kubadili tabia miongoni ma wana jamii.
Kwa mujibu wa Dk Kalinga, sera iliyopita ilijikita katika programe za UKIMWI lakini katika sera mpya iliyofanyiwa marekebisho inaweka msisitizo wa programu hizo kujenga kwa mtazamo wa kwamba inabidi zianze kwa mtu binafsi.

0 comments:

Post a Comment