Thursday, January 24, 2013

Tunataka kutembelea miradi yote ya UKIMWI-Kamati ya bunge



WAJUMBE wa kamati ya kudumu ya bunge ya katiba,sheria na utawala wametaka kupewa umuhimu wa kutembelea mara kwa mara miradi na shughuli mbali mbali zinazohusiana na kampeni dhidi ya UKIMWI nchini ili kujua hasa thamani ya fedha (value of money) zinazotolewa na serikali pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kupambana na ugonjwa huo.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao, Mh. Chana Pinda, wajumbe hao walitoa dai hilo jijini jana  walipokutana na viongozi wa ngazi za juu wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS).

“Hatuwezi kuhakiki thamani ya fedha zinazoelekezwa katika miradi ya kupambana na UKIMWI kama tutaendelea kuletewa ripoti na taarifa kwenye makaratasi tu. Tunapaswa kufika kwenye maeneo ya miradi ili kuona walengwa wananufaikaje,” alisema Mh Deogratius Ntukamazina, Mbunge wa Ngara na kiongozi mstaafu katika tume ya utumishi.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Mh.Abbasi Mtemvu, mbunge wa Temeke ambaye alisema ikiwa kamati itaendelea kutengwa katika shughuli muhimu zinazohusiana na kampeni dhidi ya UKIMWI, ni dhahiri itaendelea kupitisha bajeti ambayo huenda haiwanufashi walengwa.

Kama kamati haiwezi kufika huko kwenye miradi au halmashauri zinazopelekewa mamilioni ya pesa ili kupambana na UKIMWI kila mwaka, ni dhahiri kwamba kamati itakuwa inapitisha pesa ambazo haijui mwisho wa siku zinafanya nini, alisema Mh Mtemvu

Akisisitiza umuhimu huo, Mwenyekiti Mh. Chana Pinda alisema ziara kama hizo zitaiwezesha kamati yake kujua kinachoendelea huko kwenye jamii.

“Wajumbe wanataka ziara hizi sio kwa ajili ya posho, bali kwa ajili ya kutembelea miradi mbali mbali ya UKIMWI nchini na hivyo basi kuweza kujua kinachoendelea huko mashinani na kuchukua hatua stahiki,” alisema Mh.Pinda

Wajumbe hao walitoa dai hilo mara baada ya naibu mwenyekiti wa TACAIDS Bi Beng’ Issa kutoa taarifa ya mwenendo wa kampeni dhidi ya UKIMWI nchini. TACAIDS ndiyo mratibu wa shughuli zote a UKIMWI nchini ikifanya kazi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu

Katika taarifa yake, Bi Issa alisema  kuwa licha ya kukabiliwa na ufinyu wa bajeti unaochangiwa na kupungua kwa misaada ya wahisani, serikali ilikuwa imejipanga kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI (VVU) kwenye jamii ya kitanzania kwa silimia 9 

Ili kufikia lengo hilo pamoja na mengine, serikali ilikuwa inajipanga kuhakikisha mfuko wa UKIMWI (AIDS Trust Fund) ambao ni jitihada za watanzania wenyewe unaanza kufanya kazi vizuri.
Takribani shilingi bilioni 300 zitakuwa zinakusanywa kutoka serikalini kupitia mfuko huo kila mwaka. 

Aidha mikakati mingine ya kufikia azma hiyo ni kuhakikisha mamlaka za serikali za mitaa zinatenga fedha kutoka kwenye vyanzo vyake kwa ajili ya shughuli za UKIMWI.

“Aidha tumejipanga kuanza kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha za UKIMWI kwenye mamlaka za serikali za mitaa kuangalia matumizi kwa thamani ya fedha,” alisema Bi Issa ambaye pia ni Mkurugenzi wa masuala ya fedha wa TACAIDS.

Wakati huo huo, Kamati hiyo ya bunge iliitaka TACAIDS kuharakisha kutoa utafiti mpya wa masuala ya UKIMWI nchini ili kuwa na takwimu mpya na sahihi kuhusu ugonjwa huo. Hadi jana, takwimu zinazotumika ni zile za utafiti wa hali ya UKIMWI nchini uliofanyika mwaka 2007 na 2008 ulioonyesha kiwango cha maambukizi cha asilimia 5.7 

Akijibu rai hiyo, Bi Issa alisema tume ilikuwa inajiandaa kutoa takwimu mpya za hali ya UKIMWI nchini katika kipindi cha miezi miwili ijayo mara baada ya kukamilika kwa utafiti mpya uliofanywa na Shirika la Takwimu la Taifa (TBS)

Friday, January 4, 2013

Media Competition on the Effects and Prevention Efforts of HIV/AIDS to Youth and Women


DAR ES SALAAM, January 3, 2013: The Association of Journalists Against AIDS in Tanzania (AJAAT) in collaboration with the Tanzania Commission for AIDS (TACAIDS) is announcing a media competition on HIV and AIDS Prevention focusing on Youths and Women. This activity is being supported by the United Nations Population Fund (UNFPA)
Jumanne Issango (right) acting DAI from TACAIDS


Entitled: MEDIA COMPETITION ON THE EFFECTS AND PREVENTION EFFORTS OF HIV/AIDS TO YOUTH AND WOMEN, the competition aims to harmonize the media to write more about the impacts of HIV and AIDS to youths and women and what should be done to prevent the two groups from new infections of the virus for the betterments of the families and the nation as a whole. 
The competition that will lasts for three months—from December 31th 2012 to March 31th, 2013—will involve local journalists from print (newspapers), electronic (radio and TVs) and new media (bloggers). Strategically, the competition aims to enable the community members to recognize and motivate it to focus on the efforts that will enable the nation achieving its ambitious plan of bringing new HIV infections to Zero by 2015. This intervention is part of the activities of the United Nations Development Assistance Plan for Tanzania (UNDAP 2011-2015) in the annual work plan of the UN Programme Working Group for HIV & AIDS.

The contents of the features or items or programmes to be accepted in the competition should largely focus on how HIV/AIDS has affected youths and women (economically, socially and in terms of their health status). 
The information should, for example, show or highlight important issues for HIV prevention among the youths and  women, care & support for youths or women living with HIV and AIDS (PLHIV), as well as treatment (in terms of re-infection), family integration, resource mobilization, research and knowledge management.
A press briefing to announce the competition yesterdy
It should state why the two groups continue to be the most vulnerable to HIV and AIDS in the country and what the causes are. The features or programmes or items should, therefore, propose or suggest or highlight methods and ways to enhance HIV prevention programmes targeting women and youths.
2.0 ELIGIBILITY AND CRITERIONS: 
-     Participants to the competition are all the media practitioners in the country, or foreigners working for the Tanzania media.
-     Items or entries allowed to be submitted include, features articles, TV documentaries, Radio programmes, cartoons, photographs and blog reports
-     The entries must focus or target issues such as stigma and discrimination, why women and young people are more vulnerable, challenges met by women and young people to access HIV information, services and support and should be detailed with adequate educative information
-     The features or items should specifically focus or target the society of Tanzania
-     It should be original, and not copied from any other publications, i.e. Newsletter, Magazine, Newspaper, TV, Radio Programmes, blogs, etc.
-     It should have appeared in the media from December 31th 2012 to March 31th, 2013.
-     Languages accepted are Kiswahili or English.
-     Only original clippings or items will be accepted.
-     Submission is restricted to up three different (3) entries per journalist.
-     Deadline for submission is April 7th 2013
-     Different attractive prizes and certificates will be offered to the winners to be selected by professional judges from media and HIV/AIDS and Health circles 
Briefing continues


3.0 TARGET GROUP:
Local journalists or columnists from print, electronic and new media (i.e Newspapers, Radio, Television and Blogs)
4.0 DURATION:           
December 15th 2012 to March 15th, 2013
5.0 SUBMISSION:
Submit your entries by hand to: 
Ms. Jovina Bujulu
 Idara ya Habari MAELEZO,
Samora Avenue
DAR ES SALAAM
 Or
Send by post or hand delivery to:
AJAAT-UNFPA-TACAIDS MEDIA COMPETITION ON HIV/AIDS,
P O BOX 33237,
KIJITONYAMA, BAHARI MOTORS BLDG.
PLOT NO.43, TEL. 0713 640520/0786 300219/ 0786 653712
Link: http://www.ajaat.or.tz/home/index.php?option=com_content&task=view&id=117&Itemid=1
DAR ES SALAAM