JAJI mstaafu Mark Bomani amayatolea wito makampuni mbali mbali pamoja na mashirika ya kibiashara nchini sasa kuingia "kiukweli" katika kulisaidia taifa kupambana na tatizo la UKIMWI unaosababishwa na virusi vya UKIMWI kwa kuchangia katika kampeni dhidi ya ugonjwa huo
Wakurugenzi wa TACAIDS wakipokea hundi kutoka kwa mgeni rasmi |
Hakutakuwa na maana yoyote kwa taifa kuendelea kutegemea wafadhili wa nje kutoa misaada ya kupambana na ugonjwa ambao kwa kiasi kikubwa hauwaathiri wananchi wao bali wanaoathirika ni watanzania na familia zao ambao wengine ni waajiriwa katika makampuni au mashirika hayo
Bw. Bomani ambaye pia mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya kutengeneza bia ya Serengeti (SBL) alitoa changamoto hiyo juzi jioni wakati wa uzinduzi wa changamoto ya kila mwaka ya kuchangia kampeni dhidi ya UKIMWI kupitia kupanda mlima Kilimanjaro.
Kampeni hiyo--maarufu kama "The Kilimanjaro Challenge Against HIV and AIDS--au Changamoto ya Kupanda Mlima Killimanjaro katika mapambano dhidi ya UKIMWI"--huendeshwa na mgodi wa kuchimba madini wa Geita (Geita Gold Mine) na imekuwa ikiendeshwa kwa ufanisi takribani miaka kumi sasa
Watoto Iren na Joffrey watakaopanda mlima mwaka huu |
"Natoa changamoto kwa mashirika mengine pamoja na makampuni yote hapa nchini sasa yaanze kuchukua mkondo wa GGM kwa kuchangia bila kinyongo katika kampeni dhidi ya UKIMWI," akasema Jaji Bomani katika hafla ambayo pia ilitumika kutoa fedha kwa baadhi ya asasi tofauti zinazojihusisha na kampeni dhidi ya UKIMWI.
Tuige mfano huu kwa kuanzisha harambee za namna hii au tofauti tukilenga kutunisha mfuko wa mapambano dhidi ya ugonjwa huu--tusitegemee watu wa nje kwani nao wanachoka--wakati tatizo ni letu, akasisitiza Jaji Bomani.
Mpango wa "The Kilimanjaro Challenge Against HIV and AIDS" kwa mara ya kwanza ulianzishwa mwaka 2002 ukihusisha wapanda mlima 47 na uliwezesha kukusanya shilingi milioni 62. Hadi sasa zaidi ya shilingi bilioni 2 zimekusanywa na kunufaisha zaidi ya asasi 30 zisizo za kiserikali (NGO) zilizo katika mapambano dhidi ya UKIMWI.
Kwa mujibu wa GGM, lengo la changamoto hiyo, ni kujenga uelewa zaidi juu ya ugonjwa wa UKIMWI na VVU na kutoa msaada wa kifedha kwenye mpango huo na kujenga timu bora ya kitaifa katika mapambano hayo.
Kiongozi wa wapanda mlima Faustine Chambo akitoa ushuhuda wa kinachojiri kabla ya kupanda mlima miongoni mwa wapanda mlima watarajiwa--hofu!! |
Aidha Jaji Bomani aliwapongeza vijana wawili kutoka asasi ya Moyo wa Huruma ya Geita--Irene John (14) na Joffrey Yohana (13) kwa kuwa miongoni mwa watakaopanda mlima Kilimanjaro katika kampeni ya mwaka huu
Asasi zilizokabidhiwa fedha kutokana na kampeni ya mwaka jana (2012) ni pamoja na Moyo wa Hurum ya Geita iliyopata shilingi milioni 150. Nyingine na kiwango kilichopokelewa katika mabano ni Tume ya UKIMWI (TACAIDS)--milioni 200), Geita VCT (AMREF)--milioni 150), Mkapa HIV Foundation (milioni 50), Geita Hospital (milioni 40), na nyingine,.
Naye Mwenyekiti Mtendaji wa TACAIDS Dk.Fatma Mrisho hakumumunya maneno pale alipozea uzito uliopo mbele ya Tume na taifa kwa ujumla katika kuhakikisha ndoto ya Maambukizi ya VVU Sifuri, Vifo vya UKIMWI Sifuri na Unyanyapaa unaohusiana na VVU na UKIMWI Sifuri ifikapo mwaka 2015 inafikiwa.
Hii ni changamoto mbele yetu. Tunahitaji raslimali fedha na watu kama kweli tuna nia ya kiufikia azma hiyo, alisema Dk Mrisho na kuongeza kuwa kama makampuni na mashirika yataendelea kuona kampeni dhidi ya UKIMWI haiwahusu ni dhahiri kazi hiyo itakuwa ngumu.
Wawakilishi wa makampuni yaliyochangia fedha siku hiyo kwa kununua picha |
Akilisifia shirika la GGM, Dk Mrisho aliyachagiza mashirika mengine yaingie katika kampeni hii bila kuchelewa kwani kinyume na hapo, taifa litaendelea kupoteza nguvu kazi muhimu. Takribani shilingi bilioni 1.3 zinahitajika katika mapambano dhidi ya UKIMWI kila mwaka ingawa kiwango kinachopatikana ni chini au karibu nusu yake tu.
Kwa muijibu wa Dk Mrisho, visababishi vya maambukizi ya VVU kwa kiwango kikubwa ni watu kuwa na wapenzi au wenza wengi ki ngono na kwa wakati mmoja . Lakini pia akasema yapo maeneo mengine yanayochangia maambukizi ambayo hayajajadiliwa kwa nguvu sana kwa mfano, wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao, ukosefu wa matibabu ya awali ya watoto pamoja na masuala ya kijamii, mila na desturi
Mwakilishi wa shirika la Moyo wa Huruma la Geita akipokea hundi |
Naye Mkurugenzi wa GGM Bw. Omari Issa taasisi zisizokuwa na fedha a kujiendesha zinapata unafuu kupitia msaada huu. "Watoto waliopoteza wazazi wao kwa ugonjwa wa UKIMWI wanapata kujaliwa na kujenga tabasamu tena katika nyuso zao kupitia upendo wanaoupata," akasema Bw. Omari
Miaka mingi imepita lakini malengo ya GGM juu ya Kilimanjaro Challenge katika kuleta uelewa juu ya janga la UKIMWI ndani ya Tanzania hayatabadilika, kwa mujibu wa Bw. Omari
Baadhi ya washereheshaji kutoka Geita Gold Mine |
0 comments:
Post a Comment