- Asalamu naitoa kwa wakubwa shikamoni
Mimi ninamengi sana yale
niliyobaini,
UKIMWI gonjwa hatari
tambueni asilani,
Tondokeni tukapime
tunazidi kuchelewa.
- Naanza kwa dada zangu leo nawaambieni,
Kupima kujua afya ni
vema ndugu zanguni
Acheni vaa vimini
nakupita mitaani,
Tondokeni tukapime
tunazidi kuchelewa.
- Nakuja kwa ndugu zangu wa kiume uwanjani,
Tuacheni ngono zembe
zatutia matatani,
Pamoja na wanafunzi
waliopo mashuleni,
Tondokeni tukapime
tunazidi kuchelewa.
- Baba na mama zanguni naomba nisikieni,
Hata Babu pia bibi
naomba zingatieni,
UKIMWI hauchagui Fatuma
au Shabani,
Tuondokeni tukapime
tunazidi kuchelewa.
- Tusiwe nazo tamaa mimi nasema jamani,
Tutapatwa na maradhi
UKIMWI nambari wani,
Mtakuja kukumbuka
niliyosema zamani,
Tondokeni tukapime
tunazidi kuchelewa.
- Tusifanye ngono zembe hili tulitambueni,
Tusokote ncha kali
tukiwa matembezini
Vyachangia mambukizi ya
UKIMWI asilani,
Tondokeni tukapime
tunazidi kuchelewa.
- UKIMWI hauna dawa gonjwa hili gonjwa gani,
Lazima tujihadhari sisi
wote majumbani,
Labda tutanusurika na
gonjwa hili jamani,
Tuondokeni tukapime
tunazidi kuchelewa.
- UKIMWI umeenea mimi nasema yakini,
Haujulishi kwa macho
wewe ukaubaini,
UKIMWI sasa tishio
tunaisha majumbani,
Tondokeni tukapime tunazidi
kuchelewa.
Mtunzi: Maulidi A.
Ugama
Jina la kisanii: Ujinga
si mzigo.
Ikwiriri sanaa group,
Rufiji.
0 comments:
Post a Comment