MADEREVA wa malori ya
mizigo ya kwenda mikoani na nchi jirani sasa watakuwa hawana shida ya kupata
maarifa, elimu na hudumu mbali mbali za Virusi vya UKIMWI—ikiwa ni pamoja na
kupima kwa hiari ili kujua hali zao—kutokana na ufunguzi wa kituo cha maarifa ya
udhibiti wa ugonjwa huo jana katika eneo la Mdaula, nje kidogo ya mji wa Chalinze,
Mkoa wa Pwani.
|
Dk.Mrisho akikata utepe wa kuzindua kituo cha Mdaula |
Uzinduzi huo uliongozwa
na Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dk. Fatma Mrisho
na kushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mh. Ahmed Kipozi pamoja na
viongozi mbalimbali wa wilaya na vijiji vya Mdaula, Matuli na Mbena.
Huduma zitakazotolewa
na kituo hicho ambacho kimejengwa kwa gharama ya Sh. 57 milioni ikiwa ni
mchango wa Mradi wa Kudhibiti UKIMWI Eneo la Maziwa Makuu (GLIA) kupitia TACAIDS
pamoja na mchango wa wanajamii wa Mdaula na Halmashauri ya Bagamoyo kwa kutoa
wataalam wakati wa ujenzi, ni pamoja na ushauri nasaha na upimaji wa
VVU.
Nyingine ni kutoa elimu
na maarifa mbalimbali za UKIMWI, burudani kwa jamii kama vile luninga, michezo
ya darts na pool pamoja na huduma za intaneti.
Akizungumza katika
hafla hiyo, Dk. Mrisho alisema uzinduzi huo ulikuwa unabainisha nia ya serikali
ya kuleta huduma za jamii ikiwa ni pamoja na zile zinazohusiana na vita dhidi
ya UKIMWI karibu na wananchi.
“Nia ya serikali ni
kuhakikisha huduma zinafika karibu na kaya. Kwa mfano, wananchi hawapaswi
kuendelea kwenda mbali kufuata huduma za tiba, matunzo, upimaji au elimu kuhusu
UKIMWI. Badala yake huduma hizi ndizo ziwafuate ili kuwapunguzia mzigo wa
safari na usumbufu. Na hiki ndicho kimefanyika hapa siku ya leo,” alisema Dk.
Mrisho
Akasema, pamoja na kuwa
kituo hicho kimejengwa ili kuwapa uwepesi madereva wa malori na magari makubwa
ya mizigo yaendayo mikoani na nchi ya jirani kuweza kupata huduma mbali mbali
na maarifa ya jinsi ya kupambana na VVU pamoja na UKIMWI, wakazi wa Mdaula
pamoja na vijiji jirani nao pia watanufaika na kituo hicho.
|
Jengo la kituo cha maarifa kuhusu UKIMWI, Mdaula |
“Mbali na ndugu zetu
madereva, ni matumaini yangu pia kuwa kituo hiki kitakuwa msaada mkubwa kwa
vijana na wanawake kujipatia maarifa na elimu ya namna ya kujikinga na
maambukizi mapya ya VVU—hii itakuwa ni mchango katika kutimiza ndoto yetu ya
kutokuwa na vifo, maambukizi mapya wala unyanyapaa vinavyotokana na UKIMWI tena
ifikapo mwaka 2015,”
“Kwenu akina mama,
ukikutana na m-baba anakwambia anakutaka ki mapenzi, muulize kwanza,
umetahiriwa?, kabla hajajibu muulize tena, una kondomu??,” akaongea Dk. Mrisho
na kusababisha hadhira nzima kuripuka kwa kicheko
Eneo la Mdaula pamoja
na Chalinze ni mojawapo ya vituo maarufu mkoani Pwani ambapo madereva wa magari
makubwa na malori ya mizigo hupumzika ili kujipatia mahitaji mbali mbali kabla
ya kuendelea na safari.
Takwimu zilizotolewa
jana na Mratibu wa Mkoa wa Tume Dk. Hafidh Ameir zinaonyesha kuwa
maambukizi ya VVU katika maeneo hayo ni kati ya asilimia 9 hadi 15 (9% hadi
15%).
Aidha, imebainishwa
kwamba visababishi vikuu vya maambukizo miongoni mwa jamii hiyo na nyinginezo
hapa nchini ni kuwa na wapenzi wengi kwa
wakati mmoja (MCP); matumizi madogo ya kinga (kondomu) wakati wa kujamiana
pamoja na kiwango kidogo cha wanaume wanaotahiriwa.
Kwa mujibu wa Bw.
Renatus Kihongo, Mratibu wa Programu za Kanda za Afrika na Kimataifa wa
TACAIDS, mradi wa Kudhibiti GLIA ulianzishwa mwaka 1998 kwa ufadhili wa
Mashirika ya Kimataifa ya USAID, DFID, UNAIDS na UNHCR.
|
Mratibu wa kituo hicho Bi.Beata akitoa maelezo kwa wageni |
Madhumuni makubwa ya
kuanzishwa kwake ni kupunguza maambukizi ya UKIMWI na athari zake kijamii na
kiuchumi katika Eneo la Maziwa Makuu. Nchi hizo ni Burundi, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda. Makao yake makuu ya
Jijini Kigali nchini Rwanda.
Utekelezaji wake
unafanywa kwa kushughulikia maeneo ambayo huchangia jitihada na mikakati ya
Serikali za nchi wanachama katika kushughulikia masuala mtambuka ya
UKIMWI. Kwa kipindi cha miaka minne mradi huu ulikuwa unafadhiliwa na Benki ya
Dunia kwa ukishughulikia maeneo
|
Mgeni Rasmi Dk.Fatma Mrisho akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa kituo cha maarifa kuhusu UKIMWI, Mdaula. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mh.Ahmed Kipozi |
Katika hatua nyingine,
shirika la Family Health International (FHI360) limeahidi kukisaidia kituo
hicho ili kiweze kutoa huduma endelevu kwa walengwa.
Ahadi hiyo ilitolewa na
mwakilishi wa FHI360 katika hafla hiyo Bw. Charles Fungo ambaye shirika lake
linaendesha mradi mwingine ujulikanao kama ROADS na ambao umejikita katika
kuwafikia watu walio katika maeneo hatarishi ya kuambukizwa VVU mfano wanawake
wanaofanya biashara ya ngono na madereva