Yumo Akitanda wa CCK
Baadhi ya washiriki wa shindano wakimsikiliza kwa makini mmoja wa wasahihishaji wa shindano Bw. Benedict Sichalwe kutoka AJAAT. Kushoto kabisa ni Bw. Kivamwo, mwenyekiti wa AJAAT |
Mwenyekiti Bw Kivamwo akitoa tathmini ya shindano kwa washiriki kabla ya kukabidhi zawadi |
Mshindi kutoka Nipashe Bw.Richard Makore (kushoto) akikabidhiwa zawadi na Bw Perege Gumbo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa AJAAT |
Akiwakabisha zawadi waandishi hao, Mwenyekiti wa AJAAT Simon Kivamwo jana alisema kuwa ushindi wao umetokana na makala walizoandika na kuziwakilisha AJAAT na kupitiwa na waamuzi na kuonekana kuwa bora.
Hafla fupi ya utoaji zawadi kwa waashindi hao ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa AJAAT uliopo Kijitonyama, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam
Alisema, shindano hilo lilihusisha wanahabari 30 kutoka vyombo vya habari mbalimbali nchini waliopewa mafunzo maalum ya siku tatu juu ya uandishi na upashanaji habari utakaosaidia kutokomeza unyanyapaa na utengwaji wa watu wanaoishi na VVU kwa watu walio katika makundi maalum.
“Hili lilikuwa shindano la papo kwa papo. Baada ya mafunzo yale tuliwaaalika washiriki kuandika makala zenye vigezo vinavyotokana na mafunzo yenyewe. Nawapongeza wale walioitikia mwito,” akasema Bw. Kivamwo
Mshindi kutoka Changamoto, Bw Saidi Mmanga |
Shindano hilo lilifuatia mafunzo yalitolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za UKIMWI Tanzania (AJAAT), kwa ufadhili wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na UKIMWI (UNAIDS), yalifunguliwa na Mwakilishi Mkazi wa UNAIDS, Dk. Patrick Brenny, Desemba 17, 2013.
Katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Dr. Brenny alisema vyombo vya habari katika kazi zao za kila siku vina nguvu kubwa ya kuchangia katika kampeni ya kufikia Sifuri Tatu za maambukizo mapya VVU sifuri, vifo sifuri vitokanavyo na UKIMWI na Unyanyapa sifuri kwa watu wanaoishi na VVU ifikapo mwaka 2015.
Lengo la mashindano hayo lilikuwa kuwashindanisha wana habari kuandika makala zitakazosaidia kutokomeza unyanyapaa na utengwaji wa watu wanaoishi na VVU pamoja na walio katika makundi maalum kama sehemu ya kampeni ya taifa ya kufikia “SIFURI TATU.
Harrieth Mandari wa The African akipokea zawadi kutoka kwa Bw.Gumbo |
Umuhimu wa kuyashirikisha makundi maalum unatokana na hatari kuwa kama wanatengwa na kunyanyapaliwa, watazidi kujificha na kutopima hali zao.
Kuendelea kujificha kwa watu walio katika kundi maalum kunaweza kuongeza maabukizo ya VVU na kufanya kutofikiwa malengo ya SIFURI TATU.
Makundi haya maalumu yaliyo katika hatari kusababisha kutofikiwa malengo ya kitaifa ya sifuri tatu ni wanaojidunga sindano katika matumizi ya dawa za kulevya, wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na wenye kufanya mapenzi kinyume cha maumbile.
Bw Constantine Akitanda wa CCK na Nipashe |
Ripoti za viashiria vya Malaria na VVU ya mwaka 2012 imeyataja makundi hayo kuwa na viwango vya juu vya maambukizo ya VVU. Pamoja na kampeni ya taifa ya kukabiliana na maambukizo mapya, kama hatua sahihi za kudhibiti na kukabili kasi ya maambukizo katika makundi haya hazitachukuliwa, yanaweza yasipatikane mafanikio yaliyokusidiwa.
Bi Salome Kitomari wa Nipashe |