Thursday, June 26, 2014

Kampeni ya Linda Goli Lako yaanza Tanzania

Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa Tanzania (YUNA) kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa hivi karibuni wametangaza kuanza kwa kampeni ya “Linda Goli Lako” nchini Tanzania.
“Linda Goli lako” ni mpango wa kimataifa unaosimamiwa na Mradi wa Pamoja wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa kushughulikia UKIMWI (UNAIDS) wa kuongeza uhamasishaji kuhusu kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) duniani kote kwa kupitia michezo na sekta ya muziki.
Vijana kutoka mashirika ya UN walioshiriki katika kampeni hiyo. (kushoto-kulia) ni: Dk Yeronimo Mlawa (UNAIDS), Usiah Nkhoma (UNIC), Sawiche Wamunza (UNFPA) na kiongozi wa YUNA Tanzania (jina halikupatikana)
Kampeni ina lengo la kuongeza ufahamu wa VVU na kuhamasisha vijana kujikita katika Kuzuia Maambukizi ya VVU (Matumizi ya kondomu, upimaji virusi vya Ukimwi kwa hiari, na kupunguza
idadi ya wapenzi).
Nchini Tanzania, kampeni hii inajulikana kwa Kiswahili kama ‘’Linda Goli Lako, kavukavu nomaa’’ kampeni hii ilianza kabla ya kombe la dunia 2014 na itaendelea baada ya kumalizika kwa fainali za kombe hilo.
Lengo ni kuwafikia vijana mbalimbali kwa ujumbe tofauti wa VVU na Mpango Kabambe wa Afya ya Uzazi (SRH) kupitia michezo na vyombo vya habari.
Uhamasishaji wa kampeni hiyo hususan suala la mabadiliko ya tabia zitahusisha, pamoja na mambo mengine, matumizi ya mitandao ya kijamii, michezo hususan mchezo wa mpira wa miguu kama fursa ya kutoa ujumbe na kukuza uelewa wa vijana kuhusu masuala ya afya ya uzazi. Watoa huduma za afya ya uzazi pia watahamasishwa kupitia washirika mbalimbali ili kutoa huduma wakati wowote ambapo vijana watakusanyika kwa ajili ya shughuli za michezo.
Katika wiki ya kampeni kulikuwa na mfululizo wa shughuli za kampeni katika kuhitimisha uzinduzi rasmi wa kampeni ikiwamo vipindi vya redio na televisheni.
YUNA kwa kushirikiana na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Cha Diplomasia (CFR) na Chuo Cha Biashara (CBE) walifanya mashindano ya siku mbili ya kandanda Kabla ya Kombe

la Dunia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Hosteli za Mabibo siku ya Jumamosi Juni 7 na Jumapili 8 Juni, 2014 kwa vyuo vikuu vilivyopo Dar es Salaam.
Mgeni rasimi katika uzinduzi huo alikuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Linus Mgaya. Ujumbe wa kampeni kwa vijana ulizingatia matumizi ya kondomu kama kinga ya mambo mawili, kuzuia maambukizi ya VVU na kwa ajili ya kupambana na mimba zisizotarajiwa miongoni mwa wanafunzi wa Chuo Kikuu; ukikolezwa na ujumbe Linda Goli Lako, Kavu Kavu Nomaaa.
Wakati wa Michezo, huduma za upimaji virusi vya ukimwi kwa hiyari na huduma za Afya ya Uzazi kwa ujumla zitatolewa uwanjani hapo bure.

NACP yaja na Mwongozo wa kuhakiki na kuidhinisha matangazo ya VVU na UKIMWI

Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NACP), mwishoni mwa wiki, ulizindua mwongozo wa Taifa wa Kupitia na Kuhakiki Nyenzo za habari, elimu na mawasiliano ya kubadili tabia kwa lengo la kuboresha habari na mawasiliano yanayofanywa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na wadau wake kwa lengo la kuthibiti kuenea kwa virusi vya UKIMWI (VVU).
Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa NACP Bw. Baraka Mpora akitoa utambulisho wa mwongozo huo kwa wajumbe
NACP iliyopo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ikiwa na jukumu la kusimamia masuala ya kinga, tiba, matunzo na misaada kwenye nyanja ya UKIMWI katika sekta ya afya ncini, imezindua mwongozo huo kwa wadau wa habari, elimu na mawasiliano (IEC) na mawasiliano ya Kubadili Tabia (BCC), mjini Bagamoyo.
Sehemu ya wataalam wa mawasiliano na habari wakisikiliza kwa makini mtoa mada (hayupo pichani) 
Mwongozo huo wa kwanza kwenye sekta ya afya unalenga kuweka viwango vya kitaifa ambavyo wadau wa mawasiliano ambapo nyenzo zote za machapisho na za kielektroniki za IEC/BCC zitapaswa kuhakikiwa na idara hiyo kwa lengo la kuboresha ujumbe inayotolewa.
Lengo kubwa la mwongozo huo ni kuhakikisha matangazo yote yanayohusu kinga, tiba, matunzo na misaada kwenye nyanja ya UKIMWI yanahakikiwa ubora ili kutoa ujumbe sahihi kwa walengwa katika jitihada za serikali za kuunga mkono jitihada za wadau wanaojihusisha na afua za ugonjwa huo nchini.
Dk Mapunda akitoa nasaha wakati wa ufunguzi wa mkutano huo
Katika dibaji ya mwongozo huo, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Donan Mmbando anasema licha ya juhudi kubwa ya uenezaji na upataji wa shughuli za habari na mawasiliano kuhusu VVU na UKIMWI nchini, bado kuna baadhi ya ujumbe usio sahihi unaotolewa kwa walengwa.
"Ujumbe huo unatofautiana bado ni tatizo kubwa kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika jitihada zake za kutokomeza maambukizo mapya ya VVU pamoja na kutoa matunzo, matibabu na msaada kwa watu wanaoishi na VVU," anasema katika dibaji hiyo na kuongeza;
Majadiliano katika vikundi
"Hali kadhalika usanifu wa viwango visivyofaa vya nyenzo zinazotayarishwa, wakati mwingine hufanya iwe vigumu kwa ujumbe kufikishwa kwa usahihi kwa walengwa waliokusudiwa.
Awali, akimkaribisha mgeni Rasmi katika mkutano huo, kaimu mkuu wa kitengo cha habari elimu na mawasiliano cha NACP, Ndg. Baraka Mpora alisema mwongozo huo umetokana na miongozo ya kitaifa ya kuongeza ubora wa huduma za VVU na UKIMWI iliyotayarishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuhakikisha uongezaji ubora wa afua zote kuhusiana na ugonjwa huo unatekelezwa kwa uwiano bora.
Nyenzo zote za machapisho na za elektroniki za IEC/BCC zimekuwa na mikakati mikuu ya inayotumika kuwapasha habari na kuwaelimisha walengwa ili kuinua kiwango cha cha uelewa kuhusu VVU na UKIMWI na kuhimiza makubaliano ya tabia utakaosaidia kupunguza maambukizo mapya ya VVU na maambukizo ya magonjwa ya ngono (STI).
Dk Jesse kutoka Muhimbili akitoa mada kwa washiriki
Wakati wa kuongoza mapitio ya mwongozo huo Afisa Habari na Mawasiliano  wa NACP, Shoko Subira amesema mwongozo huo pia unatoa maelekezo ya usahihi wa matumizi ya nembo inayotumika ikiwa ni pamoja na uwekaji wa nembo ya serikali.
"Kumekuwa na tatizo la jinsi ya kuweka nembo lakini kwa mwongozo huu umeagiza Nembo ya Serikali iwekwe juu ya nembo nyingine au iwe ya kwanza kushoto iwapo nembo zitawekwa kwa ulalo na kufuatiwa na nembo zingine kwa kuwa nembo hii  ni alama ya kitaifa na ni kubwa kwa hadhi kuliko nyingine," akasema Shoko

Sunday, February 23, 2014

Wanafamilia nchini wafundwa kuhusu UKIMWI

Kamishna wa TACAIDS Sheikh Hassan Kiburwa akipima VVU katika banda la upimaji lililosimamiwa na AMREF wakati wa siku ya  familia ya wafanyakasi wa Tume jana
IMEELEZWA kwamba asilimia nane ya wanandoa wanaoishi na virusi vya UKIMWI (VVU) ni ile mwenzi mmoja kuwa na maambukizi wakati mwingine hana maarufu kama “discordant couple”
Akizungumza katika hafla ya Siku ya Familia ya watumishi wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Mwenyekiti Mtendaji wa tume hiyo, Dk. Fatuma Mrisho ametoa wito kwa wananchi kupima afya zao.
Mwelimishaji kuhusu masuala ya familia Bw. Chalila akitoa somo katika siku ya familia ya wana Tume
“Kitendo cha walio katika ndoa kutegeana kupima, mfano, mmoja kuona yuko salama na mwingine kuamini na yeye yuko salama, kinarudisha harakati za kitaifa za kukomesha maambukizo mapya ya VVU,” amesema Dk Mrisho
Amesema watu wengi hawajapima, hali inayofanya jitihada za kukabiliana na maambukizo ya VVU kuwa ngumu na kuisisitiza ujumbe wake kwa walio katika ndoa kuwa wako kwenye hatari sawa na wasio kwenye ndoa ya kupata maambukizo.
Wanafamilia
Dk. Mrisho ameyataja makundi mengine yenye kiwango cha juu cha maambukizo kuwa ni wanaotumia dawa za kulevya kwa kujidunga sindano kwani utafiti zinaonyesha nusu yao wanaishi na VVU.
Kikundi cha ngoma kikiburudisha
Akizungumzia utafiti mdogo uliofanywa katika Kata ya Kimara jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Dk Mrisho amesema utafiti huo uligundua kati ya sindano 10 zilizotumiwa na watumia dawa za kulevya, saba zilikutwa zina virusi hivyo vinavyosababisha UKIMWI.
Ameyataja makundi mengine ambayo tafiti zimegundua kuwa na viwango vya juu vya maambukizo kuwab ni watu wenye wapenzi wengi pamoja na wanaofanya au kushiriki katika kuuza ngono.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya PM Bi.Regina Kikuli akikata keki ya Tume kama ishara ya kuunga mkono malengo ya sifuri tatu dhidi ya VVU na UKIMWI
Mapema, akitoa mafunzo kwa wanafamilia wa TACAIDS, mwezeshaji, Simon Chanila alisema kukosekana kwa uaminifu katika ndoa ni sehemu ya changamoto.
Chanila amesema kukosekana uaminifu katika ndoa kunasababishwa na kukosekana kwa uwazi, uaminifu, tamaa, kutotimiziwa matarajio ya mmoja, kukosekana kwa mawasiliano pamoja na ndoa za kulazimishwa.
Wanafamilia wa TACAIDS wakiselebuka
Aliwaambia wana familia hao kwamba ili ndoa zidumu, wanapaswa kuzingatia kanuni 14 alizowaambia zikiwa ni pamoja na kumshirikisha Mungu katika hatua zote za mahusiano yao.
Kanuni nyingine ni wenza kujitengea muda, kuonyesha kujaliana, kujali tendo la ndoa, kuwa wazi, kumpenda na kumsifia mwenzake wa ndoa pamoja na kutotilia maanani watu nje ya muunganiko wao.
Msanii "Nyerere" akibadilishana na mwana-TACIDS Elisha Mngale
Chanila ametaja kanuni nyingine ni kujua majukumu, kushirikiana pamoja na kuomba msamaha na kusamehana.
Katika tuko hilo, vijana na watoto wa familia ya TACAIDS nao pia walipewa mafunzo kwa niaba ya wana rika wenzao nchini.
Mama na mwana
Mmoja wa wakufunzi kutoka tume hiyo Bw. Hatibu Kunga aliwataka vijana hao kuzingatia maadili mema ya maisha kama njia kuu ya kuepuka kuambukizwa VVU
Akipokezana na Mkurugenzi wa mwitikio wa taifa kuhusu UKIMWI wa Tume Bw. Morisi Lekule, mwezeshaji huyo alisema badala ya kujiingiza katika vitendo hatarishi wakati wa ujana, badala yake wajikite katika shughuli za mazoezi baada ya kazi za darasani na nyumbani ili miili yao iwe na afya na kutokuwa na vishawishi vyovyote vibaya.
Mwelimishaji kuhusu kinga ya VVU Bi Noela Mbeyela kutoka T-MARC akiwa na wageni waliotembelea banda lake jana katika siku ya familia ya TACAIDS.
Mbali na mafunzo hayo, pia kulikuwa na shughuli sa upimajin wa afya, VVU na msukumo wa damu (presha) ambazo ziliendeshwa na wataalamu kutoka AMREF, T-MARC na taasisi nyingine zilioalikwa.
Moris Lekule akimwaga somo kwa vijana wana-familia ya TACAIDS. "Fanyeni excersise" muepukane na tamaa

Thursday, February 20, 2014

MSD yatoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu utaratibu wa manunuzi ndani ya bohari ya dawa

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam, wakati akitoa taarifa kwa Umma kuhusu utaratibu wa manunuzi ndani ya bohari ya dawa. Kulia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD, Heri Mchunga na Mwanasheria, Domonica Meena

IDARA ya Bohari ya Dawa (MSD) iliundwa kwa sheria ya Bunge Na. 13 ya mwaka 1993. Ni Idara inayojitegemea chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambayo ilianzishwa ili kuunda, kudumisha na kusimamia mfumo ulio bora na wenye gharama nafuu wa ununuzi, uhifadhi na usambazaji dawa na vifaa-tiba, vitendanishi kwa ajili ya hospitali  navituo vya kutolea huduma ya afya nchini
Takwimu zilizopo kwa sasa  zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia  Themanini (80%) ya mahitaji yote ya Dawa,Vifaa tiba, Vitendanishi nchini vinatoka nje ya nchi hivyo taratibu za manunuzi hufuata taratibu na miongozo ya  ndani ya nchi na ya kimataifa.
Utaratibu wa uagizaji na uingizaji wa dawa ndani ya nchi huratibiwa na kusimamiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), kuwa dawa yoyote kabla ya kuingizwa chini lazima iwe imesajiliwa na Mamlaka na  hukaguliwa pindi inapogombolewa ili kuhakikisha ubora wake. Sambamba na ukaguzi huo pia Bohari inavyo vitengo vya Ukaguzi wa Ndani (Internal Audit) na Uthibiti Ubora (Quality Assurance) ili kujihakikishia zaidi  kuwa taratibu za manunuzi zinazingatiwa pia dawa zinazonunuliwa  zinakidhi viwango vilivyokwishawekwa.
Aidha taribu za manunuzi  katika Bohari kama ilivyo taasisi nyingine yoyote ya Serikali husimamiwa  na kuongozwa na sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na
kanuni zake  za mwaka 2013. Taratibu za manunuzi huanza pale ambapo kuna  uhitaji wa dawa fulani kutoka katika vituo vya kutolea  huduma ya afya nchini. Mahitaji ya dawa kutoka katika vituo vya kutolea huduma ya afya huenda sambamba na mgawo wa  fedha kwa kila kituo husika. Bohari inayo Bodi
ya Zabuni (MSD Tender Board)  kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma yenye wajumbe ambao ni wafanyakazi katika Bohari wa ngazi za juu na wenye utaalamu tofauti. Bodi  ya Manunuzi
ndiyo chombo cha juu chenye maamuzi ya manunuzi ndani ya Bohari hivyo manunuzi yote ndani ya Bohari husimamiwa na Bodi hii.
Njia  inayotumika katika manunuzi ya bidhaa ndani ya Bohari ni kwa kupitia zabuni za kimataifa na hii ni kutokana na ukweli kwamba zaidi ya asilimia 80 ya bidhaa hutoka nje ya nchi. Zabuni ya kimataifa iko wazi kwa kila mshitiri ndani na nje ya nchi bila kubagua nchi anayotoka. Kigezo cha  kwanza  kwa mshitiri  kushiriki katika zabuni ni kuwa na bidhaa yake imesajiliwa nchini na mamlaka zinazohusika na kigezo hiki cha kusajili hakina kinga  kwa mshitiri yoyote yule.
Utangazaji wa zabuni  hufuata  na kutumia  njia na machapisho ya kitaifa na Kimataifa kupitia tovuti (webistes) za Bohari (www.msd.or.tz) na ya Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (www.ppra.go.tz). Aidha tunatumia Magazeti ya kimataifa, na ya kitaifa katika lugha za Kiingereza na Kiswahili ili kuwafikia watu wote. Zabuni hufunguliwa hadharani kwenye siku ambayo ilitamkwa kwenye gazeti na washitiri au wawakilishi wao hualikwa kwenye zoezi hilo ili kujiridhisha kuwa vigezo mbalimbali ikiwapo bei iliyotamkwa na uwepo wa nyaraka muhimu vimefuatwa
Baada ya ufunguzi hufuata mchakato  wa tathmini (evaluations) kwa kutumia wataalamu huru  kulingana na zabuni husika, wakati mwingine wataalam hao hutoka nje ya Bohari kulingana na  utaalam wao katika zabuni husika.
Baada ya mchakato wa tathmni hufuata zoezi la kuwapata washindi , zoezi ambalo hufanywa na Bodi ya zabuni. Washindi hupatikana kutokana na vigezo vilivyoweka na hupaswa kutimizwa. Washitiri wote hupewa mrejesho juu ya mchakato mzima jinsi ya zabuni ilivyokwenda na matokeo yake. Bohari hutumia mfumo  uliowazi, haki na usawa katika manunuzi ili kuhakikisha kunakuwa na ushindani na thamani fedha kwenye mali ya umma.
Sheria ya Manunuzi ya Umma inalinda haki za mshindani yeyote yule ambaye baada ya kwisha mchakato anaweza kuwa na hisia kuwa Bohari ya Dawa haikumtendea haki kwani inamruhusu kukata rufaa kwenye Mamlaka ya ya Manunuzi ya Umma (PPRA) ambao huitisha nyaraka zote toka Bohari na kuzipitia na kisha huzitolea maamuzi.
Ili kuhakikisha uwazi na haki, Sheria ya manunuzi inatutaka tuchapishe katika vyombo vya habari matokeo ya washindi wa zabuni wote kila mwisho  wa mwaka.  Taarifa ya zabuni yamwaka wa fedha wa 2012/ 13 iliiyotolewa kwenye Mwananchi la tarehe 27/ 12/ 13 na la The Guardian la  tarehe 31/ 12/ 13 nairudia hapa ili kuonyesha washindi wa zabuni hizo, thamani na nchi ambazo makampuni hayo yanatoka.
Namba ya Zabuni    Aina ya Bidhaa    Kampuni iliyoshinda    Thamani    Tarehe ya kutoa mkataba    Nchi
PHARMACEUTICALS
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/04    Supply of Pharmaceuticals    Samiro Pharmacy    $ 3,379,327    12/7/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/05    Supply of Pharmaceuticals    Tata Africa Holdings Ltd    $ 177,668    12/7/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/13    Supply of Pharmaceuticals    Nirma Limited    $ 1,214,951    12/7/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/07    Supply of Pharmaceuticals    Novo Nordisk A/S    $ 1,516,643    12/7/2013    Denmark
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/14    Supply of Pharmaceuticals    Abacus Paraental Drugs Ltd    $ 2,914,336    12/7/2013    Uganda
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/03    Supply of Pharmaceuticals    SG Star Pharmaceutical Limited Total    $ 470,150    12/7/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/16    Supply of Pharmaceuticals    Bahari Pharmacy Ltd Total    $ 1,820,539    12/7/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/06    Supply of Pharmaceuticals    Planet Pharmaceutical Ltd Total    $ 846,730    12/7/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/08    Supply of Pharmaceuticals    Serum Institute of India Total    $ 953,577    12/7/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/10    Supply of Pharmaceuticals    Medopharm PVT Ltd Total    $ 386,009    12/7/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/09    Supply of Pharmaceuticals    Pyramid Pharma Total    $ 1,422,933    12/7/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/18    Supply of Pharmaceuticals    Fresenius Kabi Total    $ 1,294,587    12/7/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/01    Supply of Pharmaceuticals    Jilichem (T) Ltd Total    $ 6,473,661    12/7/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/04    Supply of Pharmaceuticals    IDA Foundation Total    $ 797,802    12/7/2013    Netherlands
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/15    Supply of Pharmaceuticals    Claris life  sciences Limited Total    $ 970,819    12/7/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/17    Supply of Pharmaceuticals    Keko Pharmaceticals Industries (1997) Ltd Total    $ 19,485,669    12/7/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/12    Supply of Pharmaceuticals    Galentic Pharma (India) PVT Ltd Total    $ 819,836    12/7/2013    India
MEDICAL DEVICES                        
IE-009/2012/2013/HQ/G/31    Supply of Medical Devices    Sutures India    $ 1,075,805    2/8/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/31    Supply of Medical Devices    Salama pharmaceuticals ltd    $ 2,583,699    2/8/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/31    Supply of Medical Devices    HV International  FZC    $ 1,168,146    2/8/2013    UAE
IE-009/2012/2013/HQ/G/31    Supply of Medical Devices    Eastern Surgical Company Ltd    $ 41,604    2/8/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/31    Supply of Medical Devices    Amatob Ltd    €109,894    2/8/2013    UK
IE-009/2012/2013/HQ/G/31    Supply of Medical Devices    Anudha Ltd    $239,501    2/8/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/31    Supply of Medical Devices    Daima Pharmaceuticals Ltd    $199,770    2/8/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/31    Supply of Medical Devices    GIMMI GmbH    €4,170,567    2/8/2013    Germany
IE-009/2012/2013/HQ/G/31    Supply of Medical Devices    Global Agency Ltd    Ts69,171,300    2/8/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/31    Supply of Medical Devices    GST Coorporation    $3,754    2/8/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/31    Supply of Medical Devices    Immunolabs Medical Supplies    $75,020    2/8/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/31    Supply of Medical Devices    Jilichem (T) Ltd    $1,044,075    2/8/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/31    Supply of Medical Devices    Lucky Exports    $2,179,765    2/8/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/31    Supply of Medical Devices    Royal Mark Supplies Co. Ltd    Ts49,402,500    2/8/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/31    Supply of Medical Devices    Tanzania Printing Services    Ts3,094,687,847    2/8/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/31    Supply of Medical Devices    Vita Foam  (T) Ltd    $746,241    2/8/2013    Tanzania
LABORATORY REAGENTS
IE-009/2012/2013/HQ/G/32    Supply of Laboratory Reagents and Equipment    Biocare Health Products Ltd    $3,321,865    2/8/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/32    Supply of Laboratory Reagents and Equipment    S.SE.M Mthembu Medicaal Pty Ltd    $497,052    2/8/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/32    Supply of Laboratory Reagents and Equipment    Surgimed Pharma Limited    $98,421    2/8/2013    Kenya
IE-009/2012/2013/HQ/G/32    Supply of Laboratory Reagents and Equipment    Immunolabs Medical Supplies Ltd    $132,480    2/8/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/32    Supply of Laboratory Reagents and Equipment    Crown Health Care (T) Ltd    $74,399    2/8/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/32    Supply of Laboratory Reagents and Equipment    Anudha Limited    $1,939,551    2/8/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/32    Supply of Laboratory Reagents and Equipment    Pyramid Pharma Limited    $313,756    2/8/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/32    Supply of Laboratory Reagents and Equipment    Jillichem (T) Ltd    $263,787    2/8/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/32    Supply of Laboratory Reagents and Equipment    Indepth Scientific Company Ltd    $200,345    2/8/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/32    Supply of Laboratory Reagents and Equipment    HV International FZC    $476,621    2/8/2013    UAE
IE-009/2012/2013/HQ/G/32    Supply of Laboratory Reagents and Equipment    Ecolat Medical Supplies    $76,396    2/8/2013    Kenya
IE-009/2012/2013/HQ/G/32    Supply of Laboratory Reagents and Equipment    Kas-Medics Limited    $58    2/8/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/32    Supply of Laboratory Reagents and Equipment    Revital Healthcare EPZ Limited.    $226,534    2/8/2013    Kenya
IE-009/2012/2013/HQ/G/32    Supply of Laboratory Reagents and Equipment    Standard Diagnostic SD (Africa) Limited    $541,528    2/8/2013    South Korea
PHARMACEUTICALS
IE-009/2012/2013/HQ/G/33    Supply of Pharmaceuticals    Elys chemical industries limited    $603,577    5/7/2013    Kenya
IE-009/2012/2013/HQ/G/33    Supply of Pharmaceuticals    Galentic Pharma ( India ) Pvt. Ltd.           $25,444    5/7/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/33    Supply of Pharmaceuticals    H V International FZC    $2,843,515    5/7/2013    UAE
IE-009/2012/2013/HQ/G/33    Supply of Pharmaceuticals    Aurobindo Pharma Ltd    $181,116.81    5/7/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/33    Supply of Pharmaceuticals    Fresenius Kabi India Pvt Ltd    $7,165    5/7/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/33    Supply of Pharmaceuticals    Claris Lifesiences Limited    $2,945,041    5/7/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/33    Supply of Pharmaceuticals    Samiro Pharmacy    $127,349    5/7/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/33    Supply of Pharmaceuticals    Vital Supplies Limited    €27,972    5/7/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/33    Supply of Pharmaceuticals     Milan Laboratories (India) Pvt. Ltd    $47,212    5/7/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/33    Supply of Pharmaceuticals    Jilichem (T) Ltd    $2,914,547    5/7/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/33    Supply of Pharmaceuticals    Medopharm    $223,421    5/7/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/33    Supply of Pharmaceuticals    Salama Pharmaceutical Ltd    $15,307    5/7/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/33    Supply of Pharmaceuticals    Guilin Pharma    $928,950    5/7/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/33    Supply of Pharmaceuticals    MacNaughton    Ts215,342,400    5/7/2013    Tanzania
                         
MEDICAL DEVICES                        
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices    IDA Foundation    $2,510,897    16/9/2013    Netherlands
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices     Salama Pharmaceuticals Ltd    $4,760,055    16/9/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices     Amatob Limited    $7,270,952    16/9/2013    UK
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices    Hebei Oriental Pharma Imp & Exp.Corporation    $143,491    16/9/2013    China
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices    HV International FZC    $486,867    16/9/2013    UAE
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices    Jilichem (T) Ltd    $4,299,625    16/9/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices    Surgimed Medical Supplies Co. ltd     $2,079,601    16/9/2013    Kenya
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices    Tata Africa Holdings (T) ltd    $370,186    16/9/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices     Vitafoam (T) Ltd     $3,052,381    16/9/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices    Anudha Ltd    $7,141,196    16/9/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices    Daima Pharmaceuticals co Ltd    $33,600    16/9/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices      Elcon Medical Instrunments GmbH    $182,190    16/9/2013    Germany
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices     Alitom Medicare Ltd    $939,722    16/9/2013    Hong Kong
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices    Crown Health care(T) Ltd    $886,173    16/9/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices     Ecolat Medical Supplies    $245,125    16/9/2013    UK
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices    Fuda Pharmaceutical Company Ltd    $200,666    16/9/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices     G.S.T Corporation Ltd    $178,643    16/9/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices    Jaffery Ind.Saini Ltd    Ts3,518,590,000    16/9/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices     NN General supplies     Ts72,770,000    16/9/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices     Pyramid Pharma    $283,710    16/9/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices    Sinoafrica Medicine and Health Ltd    $3,559    16/9/2013    Uganda
IE-009/2012/2013/HQ/G/34    Supply of Medical Devices    United Poly Engineering pvt Ltd     $700,692    16/9/2013    India
Kwa ufupi wafanya biashara wa Tanzania walipata mikataba 41 wakifuatiwa na India 19, Kenya 6, UAE 4, UNITED Kingdom 3, Uganda, Netherlands, Germany na China 2 kila moja, South Korea na Denmark I kila moja.  Kwa hiyo wafanya biashara kutoka Tanzania walipata zaidi ya 50% ya mikataba yote.
Shughuli zote za manunuzi hukaguliwa kila mwaka na wakaguzi kutoka ofisi ya PPRA na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).
Imetolewa na
Cosmas Mwaifwani
Kaimu Mkurugenzi Mkuu

Monday, February 10, 2014

Kizimbani kwa tuhuma za kusambaza ARV feki

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Limited (TPI), Ramadhani Madabida (kulia) na Ofisa Ubora wa Bidhaa wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Evance Mwemezi walipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana kusomewa mashtaka ya kuuza na kusambaza dawa feki za ARV. Picha na Venance Nestory 

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Ltd cha Dar es Salaam (TPI), Ramadhani Madabida na wenzake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kusambaza dawa bandia na kusababisha hasara ya Sh148.3 milioni.

Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi aliwataja washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo kuwa ni Mkurugenzi wa Operesheni wa TPI, Seif Shamte, Meneja Masoko, Simon Msofe, Mhasibu Msaidizi, Fatma Shango pamoja na wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD), Sadick Materu na Evans Mwemezi.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Nyigulile Mwaseba, Wakili wa Serikali, Shadrack Kimaro alisema katika shtaka la kwanza, Aprili 5, 2011, Madabida, Shamte, Msofe na Shango wakiwa na nyadhifa hizo kwenye kiwanda cha TPI walisambaza makopo 7,776 ya dawa bandia za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARV) aina ya Antirectroviral.

Kimaro alidai kuwa washtakiwa hao, walifanya kosa hilo kinyume na kifungu cha 76 (1)(2) cha Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi ya mwaka 2003, wakijaribu kuonyesha kuwa dawa hizo zilikuwa halali na kwamba zimetengenezwa Machi, 2011 na muda wake wa kutumika unakwisha 2013 wakati wakijua kuwa si kweli.

Katika shtaka la pili, Wakili Kimaro alidai kuwa Aprili 11, 2011, Madabida, Shamte, Msofe na Shango walisambaza na kuuza makopo 4,476 ya dawa bandia aina ya Antiretroviral walizokuwa wakijaribu kuonyesha kuwa zilikuwa na viambatanisho vya Starudine 30mg, Nevirapine 200mg, Lamivudine 150mg pamoja na fungu namba OC 01.85.

Alidai kuwa washtakiwa hao waliweka viambatanisho hivyo wakijaribu kuonyesha kuwa dawa hizo zilikuwa halisi na kwamba zilitengenezwa Machi 2011 na muda wake wa kutumika ulikwisha Februari 2013 huku wakijua kwamba ni uongo.

Katika shtaka la tatu wanadaiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kinyume na Kifungu cha 302 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Wakili Kimaro alidai kuwa kati ya Aprili 12 na 29, 2011, washtakiwa hao wakiwa na nia ya kulaghai, walijipatia Dola za Marekani 98,506 sawa na Sh148,350,156.48 wakijaribu kuonyesha kuwa kiasi hicho cha fedha ni malipo halali ya makopo 12,252 ya dawa aina ya Antirectrovial yaliyokuwa katika fungu (batch) namba OC 1.85.

Alidai pia kuwa washtakiwa hao walikuwa wakionyesha dawa hizo bandia zilikuwa zimetengenezwa Machi, 2011 na kwamba muda wake wa kumalizika kutumika ni Februari, 2013 na wakafanikiwa kujipatia kiasi hicho cha fedha kutoka MSD.

Katika shtaka la nne, Materu na Mwemezi wakiwa ni Meneja wa Udhibiti Viwango na Ofisa Udhibiti Viwango wa MSD, kati ya Aprili 2 na 13, 2011 huku wakijua nia ya kutendeka kwa makosa hayo ya usambazwaji wa dawa bandia, walishindwa kuzuia kinyume na Kifungu cha Sheria namba 383 cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Katika shtaka la tano, wakili huyo wa Serikali alidai kuwa kati ya Aprili 5 na 30, 2011, washtakiwa Madabida, Shamte, Msofe, Shango pamoja na Materu na Mwemezi, kinyume na Sheria ya Uhujumu Uchumi, walishindwa kutekeleza majukumu yao wakiwa watendaji.

Alidai kuwa katika kipindi hicho, washtakiwa hao kwa pamoja walishindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kusambaza makopo 12,252 ya dawa bandia wakijaribu kuonyesha kuwa zilitengenezwa Machi 2011 na kwamba zitakwisha muda wake wa kutumika Februari 2013 na kuisababishia mamlaka hiyo ya Serikali hasara ya Sh148,350,156.48.

Washtakiwa wote walikana mashtaka yanayowakabili na upande wa mashtaka ulisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Akitoa masharti ya dhamana, Hakimu Mwaseba alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao wanafanya kazi kwenye taasisi zinazotambulika kisheria na kwamba kila mdhamini angesaini bondi ya Sh6,181, 256.

Pia alimtaka kila mshtakiwa kutoa kiasi cha Sh12, 362,513 milioni taslimu mahakamani hapo au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Madabida na Materu waliachiwa huru baada ya kukamilisha masharti hayo huku wenzao wakipelekwa mahabusu kusubiri kuyakamilisha.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 24, mwaka huu itakapotajwa.  Kwa habari kamili tembelea: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Mwenyekiti-wa-CCM-Dar-kizimbani-/-/1597296/2201040/-/item/1/-/atfg3x/-/index.html

  • SOURCE: Mwananchi


Saturday, February 8, 2014

Avoid Diversions: Acha Michepuko--Sio Dili

Baki Njii Kuu, Michepuko katika ndoa haifai: avoid diversion, avoid HIV infections! Bravo PSI
The challenge ahead of us is to avoid diversions in our wedlock. Most of us have failed to concentrate with main roads (our partners--being wife or husband). It is common to see a married man sneaking out to find a short time sex partner outside of his wedlock.
Same applied to married women. They claim they want extra pleasure. What kind of pleasure that is not found at your home anyway! sic! Uhuni huo tu!. This, according to available statistics has resulted into many people in marriage become HIV positive.
The latest numbers of balloons that are strategically “dumped” at various road intersections in the city of Dar es salaam try to remind us to avoid multiple sexual partners and instead remain faithful to our wives or husbands. Bravo PSI for this interesting innovation of communication -- Tuache utani jama!--Michepuko Sio Dili!!!!
In one of the studies conducted to assess the level of prevention awareness among married couple a few years ago, it was established that most of the married partners were involved in extra marital sex. Many married partners perceived themselves to be at risk of HIV infection.
High-risk perception among married partners was not associated with taking preventive measures against HIV infection. About 70% of married partners said that extramarital sex was unavoidable. Mungu Wangu!!--My God!!
More than half of the married women who had extra marital sex did not use condoms. Condom use in extra marital sex was low. Few couples accepted faithfulness in marriage as preventive options against HIV infection.

Wednesday, January 29, 2014

AJAAT yazawadia washindi wa makala za kutokomeza unyanyapaa na kutotengwa kwa WAVIU, makundi maalum

    Yumo Akitanda wa CCK
 
Baadhi ya washiriki wa shindano wakimsikiliza kwa makini mmoja wa wasahihishaji wa shindano Bw. Benedict Sichalwe kutoka AJAAT. Kushoto kabisa ni Bw. Kivamwo, mwenyekiti wa AJAAT
DAR ES SALAAM, Januari 25, 200: WAANDISHI wa habari sita kutoka vyombo vya habari nchini wameshinda na kuzawadiwa kutokana na uandishi wa shindano la “KUTOKOMEZA UNYANYAPAA NA KUTOTENGWA WATU WANAOISHI NA VVU PAMOJA NA WALIO KATIKA MAKUNDI MAALUM” lililofanyika kati ya Desemba 20 na 31, mwaka jana.
Mwenyekiti Bw Kivamwo akitoa tathmini ya shindano kwa washiriki kabla ya kukabidhi zawadi
Waadishi walioshinda na majina ya vyombo vya habari wanakofanya kazi katika mabano ni Lucy Ngowi (Tanzania Daima), Harrieth Mandari (The African), Said Mmanga (Changamoto), Richard Makole na Salome Kitomari wote kutoka gazeti la Nipashe. Mwingine ni mwanasiasa machachari ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari Bw. Constantine Akitanda. Bw. Akitanda, kiongozi wa Chama Cha Kijamii (CCK) ameshinda kupitia makala yake aliyotoka katika gazeti la Nipashe  Desemba 28, 2013.
Mshindi kutoka Nipashe Bw.Richard Makore (kushoto) akikabidhiwa zawadi na Bw Perege Gumbo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa AJAAT

Akiwakabisha zawadi  waandishi hao, Mwenyekiti wa AJAAT Simon Kivamwo jana alisema kuwa ushindi wao umetokana na makala walizoandika na kuziwakilisha AJAAT na kupitiwa na waamuzi na kuonekana kuwa bora.
Hafla fupi ya utoaji zawadi kwa waashindi hao ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa AJAAT uliopo Kijitonyama, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam
Alisema, shindano hilo lilihusisha wanahabari 30 kutoka vyombo vya habari mbalimbali nchini waliopewa mafunzo maalum ya siku tatu juu ya uandishi na upashanaji  habari utakaosaidia kutokomeza unyanyapaa na utengwaji wa watu wanaoishi na VVU kwa watu walio katika makundi maalum.
“Hili lilikuwa shindano la papo kwa papo. Baada ya mafunzo yale tuliwaaalika washiriki kuandika makala zenye vigezo vinavyotokana na mafunzo yenyewe. Nawapongeza wale walioitikia mwito,” akasema Bw. Kivamwo
Mshindi kutoka Changamoto, Bw Saidi Mmanga

Shindano hilo lilifuatia mafunzo yalitolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za UKIMWI Tanzania (AJAAT), kwa ufadhili wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na UKIMWI (UNAIDS), yalifunguliwa na Mwakilishi Mkazi wa UNAIDS, Dk. Patrick Brenny, Desemba 17, 2013.
Katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Dr. Brenny alisema vyombo vya habari katika kazi zao za kila siku vina nguvu kubwa ya kuchangia katika kampeni ya kufikia Sifuri Tatu za maambukizo mapya VVU sifuri, vifo sifuri vitokanavyo na UKIMWI na Unyanyapa sifuri kwa watu wanaoishi na VVU ifikapo mwaka 2015.
Lengo la mashindano hayo lilikuwa kuwashindanisha wana habari kuandika  makala zitakazosaidia kutokomeza unyanyapaa na utengwaji wa watu wanaoishi na VVU pamoja na walio katika makundi maalum kama sehemu ya kampeni ya taifa ya kufikia “SIFURI TATU.
Harrieth Mandari wa The African akipokea zawadi kutoka kwa Bw.Gumbo

Umuhimu wa kuyashirikisha makundi  maalum unatokana na hatari kuwa kama wanatengwa na kunyanyapaliwa, watazidi kujificha na kutopima hali zao.
Kuendelea kujificha kwa watu walio katika kundi maalum kunaweza kuongeza maabukizo ya VVU na kufanya kutofikiwa malengo ya SIFURI TATU.
Makundi haya maalumu yaliyo katika  hatari kusababisha kutofikiwa malengo ya kitaifa ya sifuri tatu ni wanaojidunga sindano katika matumizi ya dawa za kulevya, wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na wenye kufanya mapenzi kinyume cha maumbile.
Bw Constantine Akitanda wa CCK na Nipashe

Ripoti za viashiria vya Malaria na VVU ya mwaka 2012 imeyataja makundi hayo kuwa na viwango vya juu vya maambukizo ya VVU. Pamoja na kampeni ya taifa ya kukabiliana na maambukizo mapya, kama hatua sahihi za kudhibiti na kukabili kasi ya maambukizo katika makundi haya  hazitachukuliwa, yanaweza yasipatikane mafanikio yaliyokusidiwa.
Bi Salome Kitomari wa Nipashe


Lucy Ngowi wa Tanzania Daima