Dk Mrisho akipima urefu |
TUME ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) imeyataka makampuni na waajiri nchini kuweka katika vitendo kauli ya "ukarimu huanzia nyumbani" kwa kupima afya za wafanyakazi wao mara kwa mara ili kujenga nguvu kazi imara kwa maslahi ya taifa
Wito huo ulitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti Mtendaji wa TACAIDS Dk.Fatma Mrisho wakati wa bonaza la wafanyakazi wa Tume hiyo lilofanyaka katika viwanja vya Leaders Club vilivyoko Kinondoni.
"Ni vema sasa makampuni, mashirika na waajiri wetu waweke utaratibu wa kupima afya za wafanyakazi wao mara kwa mara na wasisubiri mpaka wafanyazi waanguke kwa presha au kufariki ghafla....tusiendekeze mikutano na vikao tu na kusahau afya zetu,:" alisema Dk Mrisho katika mahojiano na waandishi wa habari waliofika viwanjani hapo.
Katika bonaza hilo lilobeba kaulimbiu ya "ukarimu huanzia nyumbani-pima afya yako" wafanyakazi wa Tume pamoja na mamia ya wakazi wa Dar es salaam waliweza kupata ushauri nasaha na hatimae kupima Virusi Vya UKIMWI (VVU) kwa hiari.
Waliongozwa na Dk Mrisho ambaye alikuwa wa kwanza kuingia katika hema la kupima. --Zoezi hilo liliendeshwa na wataalamu kutoka hospitali ya Amana ya Ilala pamoja na wale kutoka shirika la afya la AMREF
Mbali na UKIMWI, wafanyakazi hao pia walipima vipimo vya shiniko la damu au presha (BP), sukari, uwiano wa urefu na uzito (body mass index).
"Tukio hili liwe kichocheo kwa makampuni na waajiri wengine nchini," akongeza Dk Mrisho huku akisema, vita dhidi ya UKIMWI inapaswa kupigwa kila kona kuanzia ngazi ya familia, sehemu ya kazi na kwingineko ili-mradi taifa linafikia lengo la maambukizi sifuri, vifo sifuri na unyanyapaa sifuri.
Kumbe kupitia michezo na mikusanyiko kama hii, mwitikio wa watu kupima afya zao unakuwa mkubwa. Nimeona watu wengi wakijitokeza kupima afya zao...hili ni tukio kubwa ambalo halina budi kuigwa, akaongeza mwenyekiti huyo ambaye kitaaluma ni daktari
Akifafanua kuhusu tukio hilo, Meneja wa Habari wa Tume Bi Gloria Mziray amesema taasisi yake imejizatiti kuwa na matukio kama haya mara kwa mara ili kuhamasisha zaidi upimaji wa VVU mingoni mwa watanzania.
Kwa mujibu wa ripoti mpya ya utafiti wa viashiria vya VVU na UKIMWI na Malaria Tanzania wa 2011-2012 (THMIS), upimaji wa VVU miongoni mwa wanawake na wanaume ni mkubwa zaidi mijini kuliko vijijini.
Utafiti huo pia unaonesha kuwa wanawake watatu katika kila wanawake 10 na zaidi ya asilimia 25 ya wanaume wamewahi kupima VVU na kupokea majibu miezi 12 kabla ya utafiti.
Aidha ikabainika pia kwamba, upimaji wa VVU unaongezeka sambamba na ongezeko la kiwango cha elimu kwa wanaume; huku asilimia 54 ya wanaume wenye elimu ya sekondari au zaidi wakiwa wamepima VVU na kupokea majibu ukilinganisha na asilimia 32 ya wanaume ambao hawana elimu.
"Nimefurahi kuwa leo nimeshiriki katika tukio hili la kujua afya yangu. Si tukio la mara kwa mara kusema ukweli. Mara nyingi sisi tuko bize na mikutano na mipango ya kitaifa huku tukisahau afya zetu wenyewe," akasema Bi. Betty Malaki, afisa anayeshughulika na masuala ya Jinsia na UKIMWI katika Tume hiyo.
Kauli hiyo iliungwa mkono na Afisa anayeshughulika na masuala ya Mwitikio wa Kitaifa kuhusu UKIMWI Dk. Kamugisha
"Mbali na kujenga urafiki na kuchangamsha miili yetu lakini pia tumeweza kujua hali ya afya zetu. Hii inatufanya tuishi kwa kujiamini," akaongeza Bi. Salome Gerald.
Mbali na upimaji wa afya, pia kulikuwa na utoaji elimu ya matumizi ya mipira ya kiume na kike (kondomu)--Dume na Lady Pepeta--zoezi lililosimamiwa na kuendeshwa na wataalam kutoka shirika la T-MARC.
Waelimishaji, Bw. Suleiman Kombo na Bw.Seraphino Salema walikuwa na wakati mgumu katika kutoa ufafanuzi kwa wafanyazi wa Tume wa jinsi kondomu hizo zinavyotumika kwa usahihi bila kuleta madhara kwa mtumiaji.
Kwa mujibu wa THMIS-2011 na 2012, asilimia 27 ya wanawake na wanaume waliokuwa na wenzi zaidi ya mmoja miezi 12 iliyopita waliripoti kutumia kondomu mara ya mwisho walipojamiana.
Aidha, matumizi ya kondomu miongoni mwa watu wenye zaidi ya mmoja yanaongezeka sambamba na ongezeko la elimu.
Wakati huo huo, timu ya mpira wa miguu ya Tume iliibuka kidedea kwa kuilaza Clouds FM kwa magoli 2-1. Mpambano huo ambao ulikuwa sehemu ya bonaza hilo ulishuhudia Clouds FM wakiongoza kwa goli moja hadi mapumziko kufuatia shuti kali lilipigwa na straika Ephraim Elly lilomwacha mlinda mlango wa TACAIDS akiwa hana la kufanya.
Kipindi cha pili, TACAIDS, ikiongozwa na nahodha Simon Keraryo na winga mwenye mapafu kama ya mbuni, Konga, iliingia kama simba aliyejeruhiwa na kusawazisha goli dakika ya sita tu kupitia kwa Sixmund.
Dakika ya 20, Clouds FM ikiongozwa nja nahodha Shafii Dauda pamoja na kiungo mwenye mbwembwe kibao, Benny Kinyaiya walikubali goli la pili lililofungwa na Ally Mkuzo baada ya kazi nzuri ya Adebayor (rasta). Hadi mwisho wa mchezo TACAIDS wakaibuka washindi.
Hata hivyo, Clouds FM ndio walipewa kikombe kama kielelezo cha kutambua mchango wao wa kitaaluma wa kuendeleza kampeni dhidi ya VVU na UKIMWI kupitia vipindi mbalimbali vya redio. Shaffii Dauda akaahidi kuendeleza kampeni hizo kupitia Clouds FM.
Wito huo ulitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti Mtendaji wa TACAIDS Dk.Fatma Mrisho wakati wa bonaza la wafanyakazi wa Tume hiyo lilofanyaka katika viwanja vya Leaders Club vilivyoko Kinondoni.
Wafanyakazi wa TACAIDS wakipima afya zao |
Upimaji unaendelea |
Waliongozwa na Dk Mrisho ambaye alikuwa wa kwanza kuingia katika hema la kupima. --Zoezi hilo liliendeshwa na wataalamu kutoka hospitali ya Amana ya Ilala pamoja na wale kutoka shirika la afya la AMREF
Bw.Konga akijiandaa kupima huku kocha wa TACAIDS akiwa anakaguliwa tayari |
"Tukio hili liwe kichocheo kwa makampuni na waajiri wengine nchini," akongeza Dk Mrisho huku akisema, vita dhidi ya UKIMWI inapaswa kupigwa kila kona kuanzia ngazi ya familia, sehemu ya kazi na kwingineko ili-mradi taifa linafikia lengo la maambukizi sifuri, vifo sifuri na unyanyapaa sifuri.
Tukapime bwana |
Akifafanua kuhusu tukio hilo, Meneja wa Habari wa Tume Bi Gloria Mziray amesema taasisi yake imejizatiti kuwa na matukio kama haya mara kwa mara ili kuhamasisha zaidi upimaji wa VVU mingoni mwa watanzania.
Twende bwana |
Utafiti huo pia unaonesha kuwa wanawake watatu katika kila wanawake 10 na zaidi ya asilimia 25 ya wanaume wamewahi kupima VVU na kupokea majibu miezi 12 kabla ya utafiti.
Aidha ikabainika pia kwamba, upimaji wa VVU unaongezeka sambamba na ongezeko la kiwango cha elimu kwa wanaume; huku asilimia 54 ya wanaume wenye elimu ya sekondari au zaidi wakiwa wamepima VVU na kupokea majibu ukilinganisha na asilimia 32 ya wanaume ambao hawana elimu.
The dream team-TACAIDS |
Ball control |
"Mbali na kujenga urafiki na kuchangamsha miili yetu lakini pia tumeweza kujua hali ya afya zetu. Hii inatufanya tuishi kwa kujiamini," akaongeza Bi. Salome Gerald.
Mbali na upimaji wa afya, pia kulikuwa na utoaji elimu ya matumizi ya mipira ya kiume na kike (kondomu)--Dume na Lady Pepeta--zoezi lililosimamiwa na kuendeshwa na wataalam kutoka shirika la T-MARC.
Suleiman Kombo wa T-MARC akitoa elimu kuhusu kondomu |
Kwa mujibu wa THMIS-2011 na 2012, asilimia 27 ya wanawake na wanaume waliokuwa na wenzi zaidi ya mmoja miezi 12 iliyopita waliripoti kutumia kondomu mara ya mwisho walipojamiana.
Licha ya kufungwa 2-1, ni Shaffii Dauda wa Clouds FM aliyeondoka na kombe |
Wakati huo huo, timu ya mpira wa miguu ya Tume iliibuka kidedea kwa kuilaza Clouds FM kwa magoli 2-1. Mpambano huo ambao ulikuwa sehemu ya bonaza hilo ulishuhudia Clouds FM wakiongoza kwa goli moja hadi mapumziko kufuatia shuti kali lilipigwa na straika Ephraim Elly lilomwacha mlinda mlango wa TACAIDS akiwa hana la kufanya.
Kukimbiza na kukamata kuku |
Bi Mrema ndani ya VCT |
Mabingwa wa karata--hapa tupu, na hapo tupu...kalalaaa... |
RCT Chambo, tabasamu la bashasha baada ya kuibuka mshindi wa kukamata kuku |
Picha zaidi ya matukio yaliyojiri katika bonanza la TACAIDS
Mahudhurio: Dr A Mulokozi hataki mchezo, anafuatilia mahudhrio!! |
Sio mchuuzi wa kuku, la hasha, ni Dk.Kafura akifanya vitu vyake katika kusherehesha bonaza |
Timu ya Clouds FM |
Mwelimishaji wa T-MARC, Bw. Salema akitoa elimu juu ya matumizi kike, maarufu kama Lady Pepeta |
Maandalizi ya game |
0 comments:
Post a Comment