MKURUGENZI wa sera na
mipango katika Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dk. Raphael Kalinga amerejea
wito wake kwa jamii kwamba mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI yaanze kwa mtu
binafsi.
Dk. Kalinga (watatu kulia waliosimama) |
Kwa kutambua hilo, mtu
binafsi ataweka mikakati thabiti ya kujilindi yeye binafsi hata kabla ya
kumfikiria mwenza wake, familia yake na hatimae taifa lake.
Dk. Kalinga alitoa
msimamo wake huo ambao amekuwa akiusisitiza katika siku za hivi karibuni wakati
alipozungumza na mtandao wa blog ya Zuia UKIMWI Tanzania.
“Napenda nieleweke
vizuri. Ninaposema kuwa tatizo la UKIMWI ni la mtu binafsi kwanza kabla
halijawa la kitaifa, nina maana kwamba taifa haliwezi kuwepo kama hakuna mtu
binafsi. Mtu binafsi anaungana na mwenza kutengezeza familia, familia inatengeneza
jamii, baadae kijiji, tarafa, wilaya,
mkoa na hatimae taifa,” akasema Dk.Kalinga.
Kwa mujibu wa mtaalamu
huyo, kama sehemu ya kutimiza ndoto ya kitaifa ya kutokomeza kabisa kabisa kwa
kiwango cha “0” maambukizo mapya ya VVU,
unyanyapaa pamoja na vifo vinavyotokana na VVU/UKIMWI ifikapo 2015, kila
mwananchi kwa nafasi yake anapaswa kujilinda kwanza na kuhakikisha hapati
maambukizo yoyote.
Na kwa yule aliyekwisha
ambukizwa azingatie masharti ya kinga na tiba ambayo yatamfanya aendelee kuwa
mwenye siha lakini pia pasipo kupata maambukizo mengine mapya (re-infection)
Dk. Kalinga akaongeza
kuwa, kwa mtu anayemsikia haraka haraka, anaweza kuhisi kuwa anapingana na
tamko la serikali la mwaka 2005 (enzi za utawala wa Rais Mstaafu Benjamini W
Mkapa) lililoutangaza UKIMWI kuwa janga la kitaifa.
Tangu kipindi hicho,
serilai kwa kushirikiana na wadao mbali mbali katika mapambano hayo ilichukua
hatua muhimu na imara kupambana na maambukizo na kuzidi kusambaa kwa VVU na
UKIMWI miongoni mwa jamii ya Tanzania.
Mojawapo ya mafanikio
yab hivi karibuni ni kupungua kwa kiwango cha maambukizi miongoni mwa
watanzania kutoka 7.2% hadi 5.7% kwa mujibu wa takwimu za taifa za 2008/2009.
Njia zinazotumika
kupunguza maambukizi zimekuwa tofauti lakini mojawapo ni pamoja na kutoa elimu kwa
umma ya kujinga na maambukizo ya VVU , kutoa dawa kwa mama wajawazito wenye VVU
ili kuzuia wasiwaambukize watoto wanaotarajia kuwazaa, kuanzisha tiba (ARVs) kwa
watu wanaoishi na VVU pamoja na kampeni za kutahiri wanaume wasiotahiriwa
Hata hivyo, pamoja na
jitihada hizo, bado baadhi ya wananchi wameendelea kushabikia au kutekeleza
tabia ambazo zinapelekea maambukizo mapya. Mfano mzuri ni ule wa watu
kuendekeza tabia au mila za kuwa na wenza (wapenzi) wengi, maarufu kama mtandao
wa ngono.