
Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa Tanzania (YUNA) kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa hivi karibuni wametangaza kuanza kwa kampeni ya “Linda Goli Lako” nchini Tanzania.“Linda Goli lako” ni mpango wa kimataifa unaosimamiwa na Mradi wa Pamoja wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa kushughulikia UKIMWI (UNAIDS)...